Wakati niko mdogo niliwai kusikia watu/mtu akipata rupia anakuwa tajiri sana, sasa mwezi uliopita nilikuwa nasimamia mgodi wa moonston Songambele ya matui. Wakaja watu 2 kijijini wantafuta rupia, nikashangaa xana! kila nilivojaribu kuwauliza husu hizo rupia hawajawai kuziona! lakini wanasema huwa zinakuwa kwenye masanduku walioacha wajerumani na kwa hali ya kawaida huwezi kuyaona mpaka upitie kwa wazee wa matmbiko au waganga wa jadi! Sasa jamani hii kitu rupia ni kweli ipo? Ni nani anaekuwa ananunua? halafu inathamani gani? Kwa yeyote anaejua zaidi niasaidie kujua hii kitu"
yapo mengi usiyoyajua kuhusu rupia ya mjerumani,ukweli upo na uongo upo,kama unayo tuwasiliane mi nakupeleka sokoni kisha uje hapa utoe ushuhuda,kuna mengi sana na story za kuvutia kuhusu mali za mjerumani.fanya kazi kwa bidii na maarifa achana na imani za kishirikina, mimi ninayo rupia yenye picha ya simba wawili wanaangalia mnazi, ninayo zaidi ya miaka 9 sasa lakini bado sijapata mtu wa kumuuzia, wanachotaka kufanya hao jamaa ni kwamba watakuahidi kuwa ukiipata watakupa pesa nyingi sana harafu watamtuma mtu kwako akuuzie waliyonayo kwa bei ya mamilioni kadhaa na wewe kwa sababu unajua ina soko utanunua lakini ukiisha inunua tu hutawaona tena hao jamaa, unakuwa umetapeliwa kisayansi kwa maana hata ukiwaona utawakamata kwa kosa gani.
mkubwa kutapeliwa kupo kila kwenye masuala mengi yanayohusu fedwa,ila ukweli upo hiyo biashara ipo na itaendelea kuwepo ila kama hujui kitu uliza tu na utaelimishwa juu ya mambo haya ya mjerumani lakini si mchezo .Hamna lolote utalizwa tu, wapo coins collectors wanakusanya mahela ya zamani kwa ajili ya kumbukumbu, lakini ukiambiwa zinatumika kwenye mazingara unatengenezewa usawa wa kutandikwa mapesa!
mkubwa kutapeliwa kupo kila kwenye masuala mengi yanayohusu fedwa,ila ukweli upo hiyo biashara ipo na itaendelea kuwepo ila kama hujui kitu uliza tu na utaelimishwa juu ya mambo haya ya mjerumani lakini si mchezo .