Kwa wanandoa na watarajiwa

grand casual

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2014
Posts
255
Reaction score
161
[emoji427]SWALI[emoji427]

Quraan inasema
"arrijaalu qawwaamuna ala nnisaa"
je mume akishindwa majukumu ya nyumba mke afanye nini?
Hayo yote ni majukumu ya mume: Chakula kodi ya nyumba ada ya watoto shule umeme maji tiba...?

[emoji427][emoji427]JAWABU[emoji427][emoji427]

[emoji676]Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kutokana na yale aliyowapa ubora Allah baadhi yao juu ya baadhi nyingine.. "
Suratu nnisaa 34))

[emoji676]Na katika matumizi ya kupewa watoto amesema Alaah S.W: "وعلى المولود له رزقهن و
كسوتهن بالمعروف
"Na juu ya mwenye kuwa na mtoto kutoka kwa mkewe, awatimizie kuwapa rizki zao na kivazi Chao kwa uadilifu. ..
Albaqara 233

[emoji676]Na pia ikiwa mume atamwacha mkewe, basi ame amrishwa ampe kitokea nyumba
Al baqara 241))

[emoji676]Ikiwa mke ameachwa na mumewe talaka ya kuweza kumrejea, basi Anatakiwa mke huyo abaki katika nyumba ya mumewe, asitoke mwenyewe kwa hiyari yake, wala mume asimtoe kwa lazima, ila ikiwa atafanya mwanamke huyo uovu mkubwa ulio dhahiri kabisa kama zinaa na mfano wake .suratul twalaq 1 pia aya ya 6 katika sura hiyo hiyo, Allah amekataza kuwafanyia madhara wake, na ameamrisha KUWAHUDUMIA waliokuwa katika eda na wao ni waja wazito, wawahudumikie mpaka watakapozaa.

[emoji676]Na ikiwa watawanyonyeshea wanawake hao watoto wao basi watoe waume malipo ya kunyonyeshea watoto wao.

[emoji676]Na aya ya 7 baada ya hiyo imekuja amri ya kutoa matumizi waume kuwapa wake zao hata katika eda zao, kila mmoja kwa mujibu wa wasaa wake.
Na Allah ameahidi kufanya wepesi kwa mwenye kuwa na hali ngumu ya kumiliki kingi cha kutoa...

[emoji676]Na ziko hadithi nyingi sana zinaonyesha ulazima wa kutoa matumizi kumpa mke, na kuwa kutoa kwa ajili ya watu wa nyumbani ni bora kwa daraja la kwanza kabisa kuliko kutoa katika njia nyingine miongoni mwa njia za Allah.

[emoji676]Maumbile aliyoumbwa nayo mwanamke, yanalingana na majukumu aliyopewa na Allah katika uislam.
@ mwanamke ni mlezi wa watoto.
@ni mlezi pia wa mumewe.
@ maumbile yake ni ya kuwa ndani zaidi kuliko kuwa nje.
@hayalingani na kuchanganyika na wanaume Wasio jamaa katika mahram zake.
@ hayalingani na kufanya kazi nzito za kuchosha mwili kupita kiasi... nk

[emoji676]Mwanamke anatakikana kutekeleza mambo ya ndani zaidi yale yanayomuhusu mume katika kumpa raha ya nafsi, na kuhisi ladha ya ndoa.

[emoji676]Ikiwa mke atakua ni katika family zenye tabaka la juu, kwamba katika family yao wao huwa wanawekewa mfanya kazi wa ndani au mpishi, na kuwa mwanamke kwao hafanyi kazi kama hizo; itakua ni wajibu kwa mume kumuwekea mkewe mfanya kazi huyo au mpishi...

[emoji676]Ikiwa mke atatoa matumizi ya ndani ya nyumba kwa hiyari yake mwenyewe, si tatizo kufanya hivyo, na itakua ni sadaka ya kawaida. ..

[emoji676]Na mume analazimika kutekeleza mahitaji yote ya mkewe, yaliyoko ndani ya uwezo wa mume, na yanayokubalika kisheria.

[emoji676]Mume analazimika kumpa mkewe Mapambo yake ya lazima kwa mujibu wa uwezo wake. .. bila israafu wala kubakhilia.

[emoji676]Mume akiwa masikini, na mke akawa ni bora tajiri, hakuna haki ya kumlazimisha mke atoe matumizi ya nyumba...

[emoji676]Na ni dhulma ikiwa mume atamlazimisha mkewe hivyo, ila ikiwa mke atakua ametoa mwenyewe kwa hiyari yake.

[emoji676]Kuna waume wanawadhulumu wake zao kwa kuwatishia kuwaacha ikiwa hawakuchangia pesa za matumizi nyumbani, na kwa hoja kuwa mke ana uwezo...
Kuwa na uwezo mke si sababu ya kuondoka wajibu wa waume juu ya wake zao.

[emoji676]N kuna wengine huwatishia hata kuwaacha talaka ikiwa hawachangii matumizi ya ndani.
Hii ni dhulma kubwa kula mali ya mtu bila idhini yake mwenyewe.

[emoji676]Mtume S.A.W alikuwa akiwasaidia wake zake kazi za ndani, na hii si aibu, bali ni katika sunna muhimu sana kuzihuisha, bila kujali ujinga wa wajinga Wasio jua umuhimu wa kufanya haya.

[emoji676]Mke anatakiwa kuishi nae kwa wema, na huruma juu yake. .

[emoji676]Hata katika adabu za safari, Mtume S.A.W alikua akiamrisha kiongozi wa JESHI awahurumie wanawake na awapeleke kidogo kidogo, na akawafananisha wanawake kama vigae, akamwambia Swahaba aitwae Anjasha kwa kumwambia: " رفقا بالقوارير. Waonee huruma hawa vigae...yaani wanawake..

Allaahu aalam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna jipya hapo,

Kwa sababu, Mababu zetu walifanya hayo yote kabla ya hiyo dini ya warabu kuja hapa Afrika na Tanzania.

Tena matunzo, yalikuwa mazuri sana kuliko hata ya hawa waamimi wa dini hiyo baada ya kuoa kwa wakati huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…