kimboka one
JF-Expert Member
- Jan 23, 2010
- 734
- 85
Mi ninajiuliza hili swali sana sipati jibu.kwa nini kila kukicha wtz tunakuwa wajinga,tunakosa UZALENDO na ubunifu.ninasoma historia ya Mkwawa hapa jamaa alikuwa na akili sana na UZALENDO wa hali ya juu.wajerumani walipata tabu kubwa kuliko sehemu nyingine walizo tawala.sijui kwanini? hakupewa nishani ya uhuru.hoja yng kwa nini? Kizazi hiki hakuna wa aina ya mkwawa?.kadri siku zinavyo kwenda ata watu aina ya slaa hawataoneka sijui nchi itakuwa je?. Au ni haya madawa,vipodozi,net,vyakula vya makopo na tv za ughaibuni?.nisaidieni wadau.
Hapana mi nakukosoa! Kila siku zinavyozidi kwenda Watanzania wanazidi kuwa na akili, wanaozidi kuwa wajinga ni Watawala wetu ambao wanafanya ujinga wa kuwatunuku nishani kina Bibi KIROBOTO wakata hata kazi aliyonayo imemshinda!
ngojeni jkt irudi,tatizo lenu mnaongea tu kwa kuwa wengi wenu hamkupitia national service!
Mi ninajiuliza hili swali sana sipati jibu.kwa nini kila kukicha wtz tunakuwa wajinga,tunakosa UZALENDO na ubunifu.ninasoma historia ya Mkwawa hapa jamaa alikuwa na akili sana na UZALENDO wa hali ya juu.wajerumani walipata tabu kubwa kuliko sehemu nyingine walizo tawala.sijui kwanini? hakupewa nishani ya uhuru.hoja yng kwa nini? Kizazi hiki hakuna wa aina ya mkwawa?.kadri siku zinavyo kwenda ata watu aina ya slaa hawataoneka sijui nchi itakuwa je?. Au ni haya madawa,vipodozi,net,vyakula vya makopo na tv za ughaibuni?.nisaidieni wadau.
Nimefanya mengi kulingana na umri wng na elimu yng au mawanda yng ya kuwafikia.kubwa kuwaelimisha watanzania kudai haki yao na kuacha ushabiki.kimsingi unahitaji utambulisho wangu kamili ili upate rejea si maneno tuje wewe ni mzalendo? Kama jibu ni ndio ni kitu gani cha maana ambacho umewahi kuifanyia nchi yako? Kama kweli unataka watz wabadilike anza wewe usiwe kibao cha matangazo
mkuu utaendelea kuudhika tu! Kwa ukweli huuHakuna kitu kinaudhi kama hii tabia ya kujidharau. Mara sisi watanzania ni wajinga, mara sisi watanzania hatuna uzalendo! Kwa vipi? Huu ni ukoloni wa ki-fikra. Tangu jana watu wengi wamekuwa wanachambua utoaji wa nishani na kuhoji vigezo vilivyotumika kuwapa baadhi na kuacha wengine. Sasa inakuwaje watanzania wote tujiite wajinga? Au ina maana ni watanzania wote waliokaa na kuandaa orodha ya wapewa nishani? psychological scar ni hatari zaidi kuliko physical scar. Ukikazania kumwambia mtoto wako kila siku kwamba yeye ni bure hawezi kitu anaweza kweli akawa bure kwa kukata tamaa.