mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 14,192
- 19,118
Mkuu,usisahau kuja rainboot Moshi tope lake ni shida,hii michina tunayovaa utanunua kila ijumaa.Kuna swali lingine mkuu?karibu sana Rumi.
mkuu umepangiwa hapo?? ndani ya chuo ni 250,000/ kwa mwaka. nje ya chuo vyuo ni kuanzia 40,000/- , na nje unakuja chuo kwa miguu hamna nauli kama ilivyokawaida nyumba zakupanga zimejengwa karibu sana na chuo. hostels zinapatikana japo wengi hupenda kukaa nje. karibu
umemkumbusha jambo jema nguo za ajabuajabu atavaa weekend getini hatopita
Nashukuru sana kwa majibu niliyohitaji. Kuna mwanangu amechagua kuja hapo hivyo nimeona nianze mapema kuifahamu shule na mazingira yake ili nijipange kumhudumia vizuri.
Hiyo gharama ya nje 40,000/ nadhani ni kwa mwezi, na wenye Nyumba wanahitaji ulipie kwa miezi mingapi? Je wanaweza kukubali kulipia mwezi mmoja mmoja?
Hiyo nimeipenda! Imenifanya nikipende chuo!
Karibu sana mkuu,kuna vyumba mpaka elfu 25 ila ujue kutembea maana ni mbali na chuo,vyumba vya karibu be elfu 40 mpaka 70.Hostel mkuu kakupa jibu hapo juu,chakula kuanzia buku mpaka 1300,hicho cha buku full amira jiandae na kuzalisha gesi.Siasa ziache nyumbani kwenu na nguo za ajabu haswa kama wewe ni ke,kama una kitambi usijali kitaisha chenyewe maana ni seminary hapo unapoelekea.Karibu Rumi mkuu.Shule ipo mpaka uombe poo.
yaan MWECAU suruali, vinguo vifupi kupita magoti, zinazoonyesha(transparent), sijui mlegezo mwambie abebe chache maana atavaa nje ya chuo tu maana mlinzi hakubali upite akikupitisha ukakamatwa ndani ya chuo unarudishwa geti ulopitia mlinzi inakula kwake
wengi wanapenda miezi 6, chakula ni kuanzia 1000(japo hata shiba) hadi 1500 afadhali
Na hicho chumba anakuwa peke yake au wanakuwepo na wengine na kila MTU anatoa 40,000/= au wote mnaokaa chumba kimoja mnachanga ili zifike 40,000/=. Kwa maneno mengine ni sh.40,000/= kwa chumba au kwa kichwa kimoja?
Tulizindua hiko chuo wakati huo cha ualimu. Mkapa ndo alizindua
yaap kilikuwa kinaitwa saint joseph but ndo hivyo its a university now