Leo jumapili,nkaamua kupoa uswazi kwetu kichuna hakikuwa na nafasi ya kuja kututembelea,bac mama mwenye nyumba akaja kunjulia hali na stuli nkampa,baada ya kuongea hali ya hewa,siasa na vinginevyo, akanijulisha juzi alienda kwa mdogo wake huko upanga wanaishi kwa compound basi yule mdogo wa mama mwenye nyumba akampa habari dadake;;;Kisa kinaaza hivi yule mdogo mtu wa upanga anaishi yeye na mumewe hajajaliwa mtoto na housegal sasa mdogo mtu akawa analalama kweli we housegal kazi hufanyi,angalia dada mwenzio wa jirani saa1 kesha deki kesha fua we mbona mvivu,yule housegal ikawa ndo wimbo kutwa akachoka ndo kumwendea housegal wa jirani vp mwenzangu unafanyaje kazi?mbona asubuhi unakuwa ushamaliza kila kitu?bac akamwambia mm nna dawa naipaka basi ucku nawaamsha hawa hawa waajiri wangu wanafua kudeki na chai wanandaa wenyewe me nawasimamia tu.basi yule dada Mungu wake akampitia akamwambia cwezi,akarudi kugombezwa na mama cku ya cku yakamshinda akamwambia kwani huyo dada unafikiri ye ndo anafanya hizo kazi?c ndo kumpa full mkanda,basi baada ya ule mshtuko akamwita mama wa jirani na kumuuliza una kifua cndo kumwambia hausgal anachokifanya,basi wakaenda kwa mganga akampa dawa ajipake ucku alipolala akashuhudia jinsi dada wa kazi alivyokuja kuwaamsha tena kwa mateke amkeni pumbavu we baba deki we mama osha vyombo yule mama akishuhudia yote kesho yake akamjulisha mumewe akasema ucku nipe dawa,ucku akampa mumewe kupaka akalala basi ucku yule dada akaja chumbani kwao tena kuwaamsha kwa mateke yule mume akashindwa vumilia akampiga yule dada kuona hivyo akajua siri imefichuka huyo mbioooo!!!