Kuwekwe taa makaburini sio ukuta

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,557
Kwa tukio la kuhuzunisha lililotokea hivi majuzi huko pugu ningeshauri maeneo haya nyeti kuwekwe taa
Zipo taa simple sana siku hizi za kichina hizi wanazoweka barabarani ambazo zinajitegemea kwa kutumia nguvu ya jua (Solar)
Hii ingepunguza Sana matukio ya ajabu yanayokua yakitokea huko nyakati za usiku, hili nimelishuhudia Oman ambako makaburini usiku panamwangaza wa kutosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waweke taa kwani kuna shughuli inafanyika usiku huko? halafu kwa Bongo shule tu hazina umeme ambako watoto wanapata elimu ndio iwe makaburini ambako tunayaweka nje ya mji huko
 
Waweke taa kwani kuna shughuli inafanyika usiku huko? halafu kwa Bongo shule tu hazina umeme ambako watoto wanapata elimu ndio iwe makaburini ambako tunayaweka nje ya mji huko

Kutokana na hili tukio ujajifunza kitu??
 
Binadamu ukifa umekufa hauna thamani tena cha msingi tuheshimu maiti ata wakiweka taa bado wapumbàvu wachaçhe watakuwepo yapo yenye walinzi lakini bado ujinga una fanyika..
 
Naafiki sana hili la taa. Makaburini panafanyikia uchafu mwingi. Wapo wengi wanaofanya maeneo ya makaburi "gesti za bure" wanabanjuana humo. Wako wengine wanaofanyia humo uchawi- muulizeni Mshana atawaambia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkoni hoja wakiweka ukuta wataruka nawatafanya jambo lao kwa uhuru zaid maana hakuna anaye waona
Lakini wakiweka taa bila ukta itasaidia maana pata kuwa peupe na penye uwazi zaid wataogopa

👏✌
 
Kutokana na hili tukio ujajifunza kitu??
Tukio kama hilo linatokea very rare katika ulimwengu. Mwisho wa siku mtataka tuyawekee makaburi bima kama magari. Sijajifunza lolote kwenye hilo tukio na kama researcher siwezi kulitumia kama case study kufanyia judgement maana ni nadra sana kutokea na likitokea tena ujue hata kizazi chetu hakitakuwepo tena
 
Hizo taa zina bei kubwa sana sio simple kama unavyofikiri. Kuweka mfumo wa taa moja kwa maana ya nguzo, solar na bulb ni milioni 2
 

Mkuu usiseme ni nadra sana kutoke kuna matukio mangi ya hovyo yanatokea huko makabur usiku tofauti na hilo

Kwangu mm taa bado muhimu
 
kuacha uzikaji wa kisanii sanii kama ule ni suluhu toshaa kabisa na siyo kuweka mataa, matatizo mengine huwa tunayatafuta
 
Waweke taa kwani kuna shughuli inafanyika usiku huko? halafu kwa Bongo shule tu hazina umeme ambako watoto wanapata elimu ndio iwe makaburini ambako tunayaweka nje ya mji huko
✔✔
 
Au wewe ndiye muhusika Wa tukio?
 
Siko Bongo na wala sikujui huko unapoongelea nachangia kutokana na uzoefu wa nchi yangu
Kumbe ndo maana hujapata la kujifunza, huku hayo matukio ya kukuta makaburi yamefanyiwa mambo ya ajabu,
Imeshakua kero sasa lazima ufumbuzi utafutwe
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…