Ni kweli kuna makosa makubwa kwa watoa dawa kuwaelekeza wateja wao kwakutafsiri kiingereza kama kilivyo. Kiusahihi zaidi hakuna kitu kutwa mara tatu, bali mara tatu kwa siku. Ukisema kutwa mara tatu maana yake masaa 12 yenye jua, ambapo ukiyagawamasaa 12 unalazimika kunywa kila baada ya masaa manne. Ina maana kwamba kuna kipindi mwili hubaki na dawa pungufu sana mwilini kuweza kudhibiti ali kama inavyokusudiwa na wagunduzi wa dawa hiyo. Half life ya dawa ndiyo inayokutaka unywe dawa kwa tofauti ya masaa mangapi. Ama sivyo mtu angeweza kunywa saamoja, saa mbili na saa tatu akafunga siku, au aknywa kila baada ya nusu saa lakini mara tatu.
Dawa inagawanywa mara tatu katika masaa 24 ili concentration ya dawa hiyo kwenye plasma iwe stable kudhibiti hali. Dawa unayoambiwa kutwa mara tatu kwa mfano, half life yake - yaani uwezo wa dawa hiyo kupungua kwa 50% katika damu (kwa lugha nyepesi) ni masaa manane. Ili kuimarisha kiwango kilekile chenye nguvu chanya ya kuleta mabadiliko yanayokusudiwa mwilini, dawa uliyokunywa sa 1 asubuhi itakuwa imeshuka kwa kiwango cha 50% kufikia saa 8 mchana. Kwa hiyo kama unataka dawa ifanye kazi sawasawa, unapaswa kunywa tena kiasi fulani cha dawa saa nane mchana. Kwakuwa ukimeza dawa mara nyingi unachukuwa nusu saa ili ifike kwenye damu, basi kiwango kwenye damu kitapanda kufikia wakati huo, utakinyenyua tena baada ya masaa manane baadaye. Ukifuata hayo ndipo utajua kama dawa imekufaa au la.
TFDA wasijisahau, wawaambie wauza dawa kwamba wateja waambiwe ni mara tatu kwa siku nzima wakiwasisitizia na masaa yanayotakiwa. Hata mimi zamani nilijua kutwa mara tatu ndio sahihi. Hiyo ndi asili mojawapo ya kufeli kwa chloroquine hasa wapenda sindano. Akichoma mara mbili mchana analala tu usiku, resistance inazaliwa. Habari ndio hiyo kwa maneno mepesi.