Kutoka mitandaoni: Aina saba (7 ) za utajiri

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,447
AINA SABA (7 ) ZA UTAJIRI:
Unaposikia neno utajiri kitu kinachokuja akilini kwa haraka ni pesa/mali,lakin mara kadhaa tushawahi kusikia ana utajiri wa roho au ana utajiri wa watoto hizo zote ni aina ya utajiri kwamba utajiri katika maisha sio pesa tu au kumiliki mali bali mambo meng yanapojumuika kwa pamoja ndio yanakamilisha utajiri au aina za utajiri

ROBIN SHARMA anasema katika kitabu cha THE GREATNESS GUIDE 1 kwamba kama unajiita tajiri basi jitathmini unayo haya mambo 7 yakiwepo haya basi unaweza kujiita tajiri

1. UTAJIRI WA NDANI
Huu unajumuisha utajiri wa fikra,unajiheshimu vipi ,una amani na utulivu wa nafsi,?mahusiano yako na Mungu yapo kwa kiwango gani au yapo basi unapojijibu maswali haya kwa namna chanya unakuwa unamilik aina hii moja ya utajiri

2. UTAJIRI WA KIMWILI:
Afya yako ni utajiri wako hamna furaha ya mafanikio mengine iwapo afya yako ina mgogoro u mgonjwa kitandani au labda umelala tu umeparalyse au huna fahamu ,au unazuiwa kufanya baadhi ya mambo au kula aina flani ya vyakula..hivyo afya ni utajir mkubwa binadam anakuwa nao unakupa amani furaha na uhuru.

3. UTAJIRI WA KIMAHUSIANO NA JAMII/FAMILIA.
Familia yako inapokuwa na amani furaha afya njema hata weledi katika nyanja zingine unakuwa mzuri unaongezeka na utafanya vizur hata katika sehemu zingine,lakini inakuwa haina maana iwapo muda wako na nguvu zako unazitumia zaidi kuwekeza sehemu nyingine nje ya jamii yako na familia yako,unakuwa umepoteza kitu muhimu sana kwasababu hata kwenye nyakati ngumu familia ndio inakuwa karibu lakini pia hata katika uzee familia ndio inakuwa msaada wako.

4. UTAJIRI WA KAZI/SHUGHULI ZAKO.
pale unapokuwa na ujuzi ,utaalamu wa kutosha katika shughuli zako,ukazielewa,ukajua changamoto zake na ukaweza kuzitatua unakuwa tajiri katika eneo lako la kazi.

5. UTAJIRI WA KIFEDHA/MALI
Huu ndio utajiri ambao unaeleweka na wengi,unahusudiwa na kuhangaikiwa pia,ingawa pesa sio kila kitu katika maisha lakini ni muhimu kwasababu ndio inayoendesha maisha yetu ya kila siku kwa kiasi kikubwa,ukiwa na pesa basi sehemu nying ya shida zako za kila siku za maisha ambazo zinatatuliwa na pesa unaweza kuzimudu.

6. UTAJIRI WA MCHANGO WAKO KATIKA JAMII
Una mchango gani katika jamii unayoishi na inayokuzunguka au jamii zingine,umefanya mambo gani chanya katika jamii yako,jamii inakuonaje??inakuona muhimu au inakuona mzigo??majibu chanya yanakupa utajiri katika hilo.


7. UTAJIRI WA KIMATUKIO /KUFURAHIA MAISHA:
maisha yanapaswa yawe na furaha na raha za hapa na pale haijalishi unapitia changamoto gani lakin pata muda wa kufurahia maisha ,tembelea sehemu mpya,kutana na watu wapya,jifunze mambo mapya,ingiza mafunzo mapya,fanya maisha yako ya kila siku yawe bora kuliko ya jana.
 
We jifariji tu,lakin kaa ukijua namba tano ndio kila kitu hapa dunia hata mungu analijua hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…