Advocate Rwankomez Bushoke Batamuzi, Mhaya wa Ruita Muleba ameenda kwenye harusi ya Muganyizi Byejumula Mulokozi, alivyotaka kuegesha gari yake ikawa hivi:-
Mhaya – nionyeshe wenye Harrier wanapaki wapi?
Mlinzi (Bageni Bigacho) – lete huku nikuonyeshe. Paki palee…
Mhaya – maweee! Wewe Tarishi! Mbona kuna Vogue na VX hapa?
Mlinzi (Bageni Bigacho) – VX ni la Mpishi wa chakula cha harusi na Vogue ni la Karani wa kitengo cha majitaka cha Manispaa. Ni watu wa kawaida tu hao usiogope.
Mhaya – what do you mean?!
Mlinzi (Bageni Bigacho) – mimi sijui lugha wewe paki hapo.
Mhaya – impossible kwa kweli, ebu nionyeshe wenye full-tank wanapaki wapi?
Mlinzi (Bageni Bigacho) – siyo kazi yangu kuingia kwenye matenki ya magari kujuwa kuna lita ngapi.
Mhaya – basi nionyeshe Ma-advocate wanapaki wapi?
Mlinzi (Bageni Bigacho) – mbona tunachoshana! Au hutaki kupaki?
Mhaya – hapana…, sikiliza…, ukichoshwa ndiyo unalipwa ujira, kazi yako ni kuchoswa, au hujui?
Mlinzi (Bageni Bigacho) – sasa nikusaidieje mpaka hapo?
Mhaya – nionyeshe wenye Masters ya UK ya Sheria wamepaki wapi. Usinipeleke kwa mafisadi.
Mlinzi (Bageni Bigacho) – subiri hapo nikuitie Kamanda wewe.
Mhaya – ngoja…, ngoja kwanza…, basi napaki hapahapa, lakini huko ndani ukumbini unionyeshe wanaoongea Oxford English kama mimi wamekaa wapi. Usinipeleke kwa washamba Wajaluo wanaoongea Cambridge English.