Unaweza mkuu, lengo kuu la chuo kikuu huria ni kuwapa nafasi ya kusoma watu wote wenye nia hiyo hasa wakiwa hawana nafasi ya kuhudhuria masomo kwa muda wote (full time).
Unaapply ukipata unaenda kufanya registration .Ukilipia nusu ya fee unapata akaunti kwenye mfumo wao wa kujifunza unaitwa Moodle.Hapo utapata materials zote na pia hard copy unaeza pata.Kuna majukwaa ya discussion ,Kuna assignment huko.Mitihani Kuna annual na test hizo ndo zinaamua upate grade gani kwenye kozi.Ada Ni kwa unit na unit moja ni 60000Tshs.Nilipiga LLB 3 years kwa fee kama ya 3M na kidogo.
Mimi pia nilisoma utawala miaka 8 iliopita, mwaka jana nikapata shauku ya kutimiza ndoto zangu kwa kusomea Sheria. Nilijiunga na Open university kwasasa nipo second year shule inaenda vizuri.