Muda si mrefu tumemaliza conference yetu ya kwanza kabisa.
Webcast ya leo wal;iohudhuria walitoka UK,China na Afrika ya kusini,hivyo tunapenda kupata maoni toka kwa walio nyumbani,sababu gani zimewakwanza au kuwatatizo kuhudhuria conference ya leo.Tulizungumzia sana juu ya kuweka misingi thabiti kwa ajili ya webcast zijazo kwani safari ndio imeanza.yafuatayo ndio yalijadiliwa.
1.Kuhamasisha wanajamii zaidi juu ya ushiriki wa hizi conference.
2.Kuboresha njia za ushiriki wa conference,kwani kuna wadau walishindwa kushiriki kwani kwa watu wanaotumia kompyuta za cafe ingewawia ugumu zaidi kuweza kushiriki kutokana na kutoruhusiwa kusimika programu.
3.Kubadilisha muda wa conference toka saa kumi jumamosi hadi saa nane ya kila jumapili(Saa za Tanzania).
4.Kutengeneza Group ambayo itakuwa inapokea Updates za conference zote zinazofanyika,ikijumuisha dondoo na maazimio.
5.Mapendekezo ya conference ijayo ambao wadau walipendekeza iwe ni ya kupanga maazimio ya pamoja.
Hatukuweza kurekodi kwakuwa kuna baadhi ya wadau walichelewa kuingia online.Hivyo ni dhahiri kuwa kuanzia wiki ijayo wengi wetu tutashiriki zaidi na mazingira ya ushiriki yatakuwa rahisi zaidi kwa watu wa maziingira yote.
NItapost agenda ya wiki inayokuja siku si nyingi ili wadau wapate muda wa kujiandaa.
AfroIT Group