Wadau,
Kama tulivyomsikiliza Rais Kikwete Kuwa kura ya maoni itafanyika April mwakani na jinsi ninavyoona hilo lazima walitekeleze ukizingatia mizengwe iliyotawala wakati wa kupitisha hiyo rasimu.
CCM wanajua fika Kuwa Rais ajae anaweza asilipe kipaumbele hilo suala la kura ya maoni na pengine mchakato wote kuanza upya kwa hiyo watafanya lolote wawezalo ili kuipitisha katiba kabla JK hajaondoka madarakani.
Kwa maoni yangu Jambo hilo japo linapingwa na watu mbalimbali wakiwemo hata wana CCM wenyewe,lakini kundi la akina Sita hawataki kukubali Kuwa walivurunda hivyo katiba mpya lazima ipite kwa halali ama kwa haramu.
Mtazamo wangu ni kuwa endapo suala hilo litaendelea kulazimishwa ndo kitakuwa kitanzi Cha CCM kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Sababu ya kuamini hivyo ni ukweli Kuwa katiba hii haiwezi kupita bila kuchakachua kura kama ilivvyokuwa katika Bunge maalum la katiba.
Uchakachuaji huo utaamsha hasira zaidi kwa wananchi na kuiadhibu CCM kupitia sanduku la kura kwani huko watakuwa na uhakika wa mawakala watakao linda kura zao.
Jambo la msingi kwa upinzani ni kuchunguza mianya yote ya wizi wa kura na kuiweka wazi mapema. Kwa maana nyingine kura ya maoni itawezesha wapinzani kujua mbinu mpya za kudhibiti wizi wa kura jambo litakalokuwa kitanzi shingoni mwa CCM.
Nawasilisha.
Mwasilishaji unayeamini kura ya maoni itakuwa kitanzi kwa CCM 2015, hakika unaota ndoto ya ndaria kama si ya alinacha......sheria inamtaka rais aitishe kura ya maoni ndani ya siku 84 tangu alipokabidhiwa katiba pendekezwa....wenzako tunawaelimisha wananchi na hasa wapiga kura wetu katiba ilivyowajali na wengi wanapokea elimu yetu.....wewe unabaki ku-speculate tu na kuwasingizia akina sita na Chenge na umeenda mbali kuzusha uchakachuaji.....kama wewe ni expert wa kuchakachua basi chakachua ili watu watakaopiga kura ya hapana wawe wengi na SISI WA NDIYO TUWE WACHACHE....Lakini huwezi na haiwezekani kuchakachua kura kwani ninyi mnakuwa na mawakala wenu vituoni na kura zinahesabiwa vituoni hivyo wakala wenu akimaliza kuhesabu anajua kama mmeshindwa au mnaongoza...UZUSHI MWINGINE WA KITOTO MNO

Kama mlishindwa kulinda kura 600, mtaweza kura milioni 6! Watanzania hatujitambui. Upinzani Tanzania ni kama njaa ya mbayuwayu.
Mwasilishaji unayeamini kura ya maoni itakuwa kitanzi kwa CCM 2015, hakika unaota ndoto ya ndaria kama si ya alinacha......sheria inamtaka rais aitishe kura ya maoni ndani ya siku 84 tangu alipokabidhiwa katiba pendekezwa....wenzako tunawaelimisha wananchi na hasa wapiga kura wetu katiba ilivyowajali na wengi wanapokea elimu yetu.....wewe unabaki ku-speculate tu na kuwasingizia akina sita na Chenge na umeenda mbali kuzusha uchakachuaji.....kama wewe ni expert wa kuchakachua basi chakachua ili watu watakaopiga kura ya hapana wawe wengi na SISI WA NDIYO TUWE WACHACHE....Lakini huwezi na haiwezekani kuchakachua kura kwani ninyi mnakuwa na mawakala wenu vituoni na kura zinahesabiwa vituoni hivyo wakala wenu akimaliza kuhesabu anajua kama mmeshindwa au mnaongoza...UZUSHI MWINGINE WA KITOTO MNO
Umerogwa wewe unamuelimisha nani?labda ukawaelimishe mamburula wenzako wa ccm maana mlikuwa mnatunga katiba ya ccm na siyo katiba ya nchi.mimi nitapiga kura ya HAPANA.