Wakuu,
Ninakunywa maji mengi kwa siku, lita 7 hadi 10. Nafahamu kwamba inashauriwa kwa siku mtu unywe maji yasiopungua lita 3. Je kuna madhara yoyote kiafya kwa kunywa maji yanayozidi kiasi hicho?
NB: Nafanya mazoezi ya viungo kwa wastani wa saa moja hadi moja na nusu kwa siku mara tano kwa wiki.