Kunguru hafugiki

pipi mti

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
764
Reaction score
515
Wakuu mambo vipi!

Basi mwenzenu leo nimekumbuka nilivyoponzwa na yule muhenga aliyesema mapenzi ni maua popote huchanua.

Nilikua mteja mzuri sana wa bar moja huko songea maeneo ya msamala.Na hapo ndio nikajikuta katika kitanzi cha penzi la bar maid.Nilianza vizuri tu kwa kumuapproch kama wanawake wengine ivyo akaniona wa pekee sana maana wengine wote hua wanaulizia bei ya k.kitu kingine ni zile chenji zangu ambazo hua namuachia ndio zikafanya shughuli isiwe ngumu sana.Basi tukaelewana na baada ya kudumunaye kama miezi miwili nikajihisi tayari nimembadili na ninauwezo wa kumbadili zaidi awe mama bora chini ya himaya yangu.Nikamvuta getto,nikamuachisha kazi ya bar na nikamfungulia bucha ya kuuza samaki wakati mipango mingine ikiendelea.Alifanya vizuri katika biashara hiyo, baada ya miezi mitatu nikaona haina haja ya kumsimamia ivyo nimuache ajiendeleze mwenyewe.

Nilipata safari ya kwenda china(kufunga mzigo katika biashara zangu), cha ajabu nikakuta yule mbuzimawe kauza kila kitu kuanzia getto,akaenda dukani kwangu kadanganya nimemuagiza sh 4m. Na vijana wangu wa kazi walivyokua mbulula hata hawakunipigia simu kuniuliza kabla ya kumpa eti kisa wanajua ni mke wangu, hadi bucha ya samaki kabeba kila kitu na haijulikani alipoelekea.Kiukweli alinirudisha nyuma mno lakini kama mwanaume Nikajipanga upya na maisha yakaendelea.

Baada ya miaka kadhaa kupita nimekuja kumkuta bar fulani hapa dar es salaam anahudumia na usiku anauza k.Inasemekana pesa zote zile alikula bata na hakuna alichofanya.Hadi muda huu bado hajaniona wala hajajua kama nafahamu sehemu anapopatikana.Nimfanyaje mtu kama huyu?
 
kaka mkubwa pipi mti hio tunaita ajali kazini kaka, pole sana kwa masahibu hayo yaliyokukuta na katika zama hizi za kukaza kwa irons hio kwa hesabu ya haraka haraka si chini ya 10M hasara. Lakini mkuu hasara roho tu hela inatafutwa. Enjoy life mkuu, visasi na mabalaa ya kazi gani maisha yenyewe mafupi haya? utaanza kufikiria visasi... ni kupoteza mda tu na wewe ni Gentleman. Nenda kamsalimime na mpe pongezi kwa aliyokufanyia. Maisha na yaendelee.
 
Mnaonaga wanaotuma posa kwao na mwanamke ni wajinga eh ?
Bora alichokufanya !

Hiv ulishawahi kijiuliza mtu mliyekutana kwa mazingira hayo ikitokea akafia geto nini kinatokea ?

Ulichofanya sio kitendo cha k'iume kama ulimpenda ungetuma posa kwao ndugu pande zote mbili wakafahamiana hata Mungu angekubariki.

Kwa hio kwa kua umeshajua alipo na yuko bar kamnunulie beer
 
Ujinga wako mwenyewe Mkuu..
 
Jombaa we si juzi tu wamekula mtaji wako wa korosho umebadilisha biashara saiv unaenda china
 
Mchukue tena uende nae gheto, maana unaonekana wewe ni aina ya wale Madomo Zege, itakuwa umefanya juhudi kweli kumtafuta..!

Kweli KIPENDACHO ROHO...
Na Mfa na Maji...
 
Usiweke tumaini lako kwa binadamu yeyote coz wanabadilika kila uchwao...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…