Kuna mapiganio makali monduli?

Tall

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2010
Posts
1,425
Reaction score
168
Kuna taarifa ambayo haijathibitishwa kuwa kuna mapigano makali mjini Monduli mkoani Arusha yaliyotokea jana kuanzia majira ya jioni. Mapigano hayo ni kati ya Polisi na wamasai.Mtoa habari ameeleza kuwa kuna vifo vimetokea vinavyotokana na mapigano hayo.
Chanzo cha ugomvi huo inadaiwa ni kundi la ng'ombe wa wamasai walioingia katika eneo la shule ya sekondari ya serikali ya Engutoto iliyopo mjini Monduli.
Inadaiwa kuwa Polisi baada ya kupewa taarifa,waliwazuia hao ng'ombe jambo ambalo wamasai hawakulikubali na kutaka kuwachukua ng'ombe wao kwa nguvu.Masai wakawa wanatumia silaha za jadi na polisi nao wakawa wanatumia silaha za moto.Hadi sasa haijaeleweka kama hali ikoje,kama mapigano yalisitishwa jana au wamasai wanaendelea kujipanga ili usiku tena waanze kupambana.
Wana JF wa Arusha na wengine WOTE tupeni usahihi wa taarifa hii na je bado mapambano yapo au?...............NILIKUWEPO
 
waache wao si wanataka kuendelea na lowasa wao
 
hapana hakuna mapigano yoyote so far.... niko karibu sana na eneo la tukio na sijasikia chochote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…