IIla watu wanakera sana, Diamond kaza buti na ongeza love kwa yule umpendae maneno hayaondoi uhai wa mtu. Alisemwa mama yako kabla hajawa na uhusiano na mama yako kuwa hawaendani na baba yako. Walipoishi pamoja wakasema amempa limbwata. Alipobeba mimba yako wakasema mimba haijamkaa vizuri na wala sio ya mume wake (mzee abdul).
Ulipozaliwa wakasema hujafanaa na baba yako. Ulivozidi kukua ukafanana na baba yako wakasema hutakua lazima mama yako akutoe kafara. Ulipokuwa mtu mzima wakasema hutafanikiwa utakuwa maskini. Ulipofanikiwa wakasema utafulia. Ulipompata Wema wakasema unatembelea nyota ya Wema.
Mmeachana wanasema bila Wema huishi, walipoona hujapata mtoto wakasema huna mbegu za uzazi. Sasa ukampata Zari wakasema umefata pesa na anakubemenda na hutapata mtoto. Amepata mimba wanasema sio yako.
Akizaliwa anafanana na wewe watasema ngoja tuone kama watadumu na Zari na bado watasema; watasema, watasema tu hata ukimpata mwingine watasema tu, so akili kichwani kwako. Usithubutu kufata maneno ya watu, ishi the way unataka, i'm done...