Kumbe bado CCM kuna makundi?

Mududu

Member
Joined
Mar 31, 2011
Posts
71
Reaction score
36
"Kwahiyo ndugu zangu, huu ni wakati wa kuyaua rasmi makundi. Uchaguzi umekwisha na sasa tuchape kazi. Na chama hakitamvumilia mtu yeyote atakaye endeleza makundi makundi". Ni baadhi ya ujumbe uliopatikana kwenye sehemu ya hotuba ya Ndugu M/kiti wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli.

Kauli inaonyesha makundi amabayo yalikuwepo ndani ya CCM kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, bado yapo na M/kiti ipo haja sasa ya kutumia taratibu, kanuni na sheria ili kumshughulikia yeyote atakaye yaendeleza. Nimefurahi kwamba hawa watu watashughulikiwa maana kama mnataka kwenda mbele, basi ni lazima WOTE muwe wamoja. Hata hivyo, katika maisha ya uhalisia, hili ni gumu sana kutokea.

Katika chama kinachijinadi kuwa na demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, kama alivyotanabaisha katibu wao mkuu, sikutegemea kuona hapatakiwi watu wenye fikra tofauti na kiongozi, au kupenda mtu mwingine tofauti na kiongozi. Tumexzoea kusikia tuhuma hii wakipewa vyama vingine, hususani CHADEMA, lakini kinyonga anachoweza ni kujibadirisha rangi tu lakini hawezi kuwa mjusi.

Hapa swali la msingi ni kwamba, kama bado kuna watu wanampinga mkuu ndani ya chama, inakuwa watanzania wengine wote nje ya chama wanamuunga mkono. Na akitokea anayempinga anavuliwa uzalendo? Au,,,kama kuna kupingana ndani ya chama, inakuwa tufike kwenye uchaguzi 2020 kukiwa hakuna upinzani. Kauli hizi zinatolewa kumzaamzaa tu sasa hivi ila zitaweza kuwa na maana baadae, kama alivyotabili Ndugu Makamba zamani juu ya ubatizo wa moto.
 
Mkuu humu kwenye mtandao ndio wanajifanya wapo wamoja..

Lakini ndani ya hiki Chama cha Manunuzi kuna makundi mabaya na hasimu ambayo hayana mfanowe..

Na ndio maana Mkiti wao amewaambia hivyo maana anajua makundi yapo na kwamba hata yeye ndani ya chama anapigwa vita sana tu.
 
Wewe naona huelewi siasa, yaani uwe na kiongozi ndani ya Chama unachoongoza anapinga kila kitu na kuhujumu mipango ya maendeleo ili uonekane haufanyi vizuri, halafu umuache eti kwa kuwa, Chama kinahitaji kuwa na watu wenye mawazo mbadala? Nyie ndio mnaofanya hata Vyama vya Upinzani kupoteza umuhimu wao kwani watu making huwa wanashindwa kuelewa ni nini msimamo wenu kwenye burning issues.

Ndugu tofautisha kati ya kukosoa suala moja moja linapofanyika tena kupitia utaratibu wa Chama dhidi ya kebehi na hujuma za kimakundi kwa utawala uliopo madarakani.

Hebu fikiria kwa mtu mwenye akili hawezi kupost kama Nape alivyopost kukejeli ununuzi wa Bombardier kwa kusingizia wananchi wake wa vijijini kuwa Hawaii maana yake.

Leo hii tuna maeneo mengi ya kiutalii yakiwemo ya huko kwao Kusini kama visitation vya Mafia, Magofu ya Kilwa Kisiwani, miji ya Kilwa Masoko, pamoja na fukwe nyingi - hao watalii watafikaje huko kama mna wabunge wasio na maono ya hata vitu vidogo?
 
Baada ya Kila Uchaguzi uwe wa Ngazi ya Serikal au wa Ngazi ya Chama Makundi hayakosekani!

CCM imetoka kwny Uchaguzi Mkuu wa Ngazi ya Chama Nchi nzima hivyo kuna waliokosa na kupata na hivyo uwezekano wa Makundi haukosekani na ni jambo la kawaida!

1995 baada ya Jakaya kutangazwa kuwa kashindwa kwenye duru ya Pili baada ya kwanza kumshinda Mzee Mkapa na Mzee Msuya alitakiwa na Baba wa Taifa atoe neno la Shukran nae bila ya hiyana alitangaza ' kuanzia Usiku huu natangaza rasmi kufanya Kundi langu kuwa kundi la Ndugu Benjamini William Mkapa kuhakikisha tunashinda Uchaguzi Mkuu'!
 
Mku hao nao ni binadamu kwa wana haki kukosoa lilotofauti na mazingira
 

Kama ni hivyo kwamba nje wanaonyesha kuwa wapo pamoja basi ni wakimavu kiakili na kimitazamo sema wanayumbishwa na mathnbo yao.
 
Alliances ziko kila mahali,hizo hatuwezi kuzikomesha na mimi niseme kwamba ni vizuri zikawepo ili kuleta msukumo mpya na maendeleo chamani.Kudhani kwamba makundi siku zote ni mabaya sio sahihi.Hata hivyo ziwepo ili kuleta mawazo mbadala yenye nia ya kukijenga chama na taifa kwa ujumla sio kukibomoa.
 
Najiuliza hili swali bila kupata majibu. Hivi ina maana ishara ya kupendwa na kukubalika Tanzania ni lazima uambiwe na wanasiasa tu? Yaani kipimo ni mwanasiasa? Maana naona wanasiasa makundi kwa makundi ndio wanaoeneza upepo wa mtu fulani kupendwa na kuungwa mkono. Ninachojua katika maisha watu wapo kwenye nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii,n.k. Mbona tumeweka kipimo chetu cha kuungwa mkono kwa watu walio katika uwanja mmoja tu wa Siasa? Mbona sioni madaktari, maprofesa, wahadhiri, walimu, askari, wakulima, wafugaji wakiacha kazi kumuunga mkono huyu ndugu yetu malaika? Hapa unahitajika utafiti wa kujibu maswali haya:
1. Yeye ni wa makundi yote na anafanya kazi kwa ajili ya makundi yote, sasa ni kwa nini watu wa kundi moja tu waonekane wapo tayari kuacha kazi zao zinazowaingizia kipato ili kumuunga mkono?
2. Kwa nini makundi mengene hayajaona umuhimu wa kuacha kazi zinazowaingizia kipato ili kumuunga mkono huyu ndugu? kama kipo, kwa nini hajakifanya kwa makundi mengine?
3. Nini cha pekee ambacho huyu mtu amewafanyia watu wa kundi hili linaloona ni vema kuacha kazi ili kumuunga mkono?
4. Nini mtu huyu hajakifanya kwa makundi mengine kiasi cha kuwafanya watu wa makundi haya wasione sababu ya kumuunga mkono kwa kuacha kazi?
 
Assertion yako si kweli mkuu.Nimeona on several occasions vikundi vya waendesha boda boda,wasomi,wakulima na viongozi wengi wa dini wakisema wazi wazi how satisfied they are na utendaji wa Rais Magufuli.Notably absent hata hivyo kwenye kumpongeza rais ni wafanyibiashara na wafanyakazi wa serikali na mashirika ya umma for obvious reasons.Hawa watu ndio walioshiriki sana katika kuihujumu nchi na vita ya kiuchumi inayoendelea inawahusu wao moja kwa moja na imewa-affect wao zaidi kuliko makundi mengine,ingawa hata ndani ya CCM wapo cadres wengi ambao wameguswa na ambao wataguswa na vita hii.So their reaction is not unexpected.Be realistic mkuu chuki na wivi havitakusaidia sana,sana sana vitakudhuru wewe mwenyewe.Try to be positive,you will leave a healthier life.
 
CCM KWA SASA IMEJIKITA KATIKA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO, HAKUNA UBABAISHAJI KAMA WA HUKO CHAGADEMA
 
areafiftyone: Hao bodaboda na wengine uliowataja kuwa wanamuunga mkono wameacha kazi? Au "wana muunga mkono" huku wakiendelea na kazi zao? Kwa ni kumuunga mkono mtu lazima uache kazi yako? Labda huko waliko kama wangefukuzwa kwa kumuunga mkono basi hapo pangekuwa na hoja. Vinginevyo ni ufisadi kuiingiza nchi kwenye uchaguzi unaoigharimu nchi mabilioni ya fedha
 
Je aliyesema ccm kuna makundi ni cdm au mwenyekiti wa ccm imekuuma sana kwa rais kusema ya kuwa ccm kuna makundi
 
Mleta mada unataka tukusaidie kufikiri? Eti nje ya chama watu wote wanamuunga mkono!!!! Hizi nguvu nyingi na matumizi ya dola yanatoka wapi kama anaungwamkono na kila mtu?
 
inawezekana mawazo tofauti yakawepo lakini vikundi vya kinafiki marufuku.
 
Mku usajili wa chama kipya ndani ya chama utakosa vipi makundi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…