Kulinganisha gharama za tofali

the locksman

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2012
Posts
1,104
Reaction score
357
Habari wakuu wote,

Naomba kufahamu ipi ni gharama kubwa kwa ujenzi hapa Dar es Salaam, kufyatua au kununua zilizofyatuliwa tayari.
 
Naomba wenye experience wanisaidie, najua wengine ni mafundi, wengine wamejenga kwa njia hizi zote mbili. Tusaidiane wakuu.
 
Nakupa gharama zangu, nimefyatua tofali 2400.
Kukodi mashine 50000/=
Fundi kila tofali kufyatua ni tsh. 150/=(tulivyoelewana) jumla ni 360,000/=
Mifuko ya cement ilikuwa 71 jumla yake 923000/=
Usafiri mifuko ya cement sh.50,000/=
Mchanga Lorry 8 kubwa jumla sh, 420,000/=
Gharama ya maji ilikuwa bure.
gharama zote ni kama sh.1,803,000/=

Kama ningeamua kununua moja moja, tofali 2400.
Kila tofali linauzwa sh.1000, hivyo jumla ingekuwa 2,400,000/=
Kubeba na kushusha kila tofali ni sh.200/= ingekuwa jumla ni 480,000/=
Usafiri wa tofali zote trip kama 8 hivi kila trip sh.50,000/= ingekuwa 400,000/=
Jumla gharama zote kununua ingekuwa 3,280,000/=

Hivyo kwa ujenzi wangu niliokoa kama kiasi cha sh.1,477,000/=Hela ya fundi kunijengea boma

Conclusion: gharama hizi inategemea location, ulinzi nk. piga mwenyewe hesabu lakini kufyatua mwenyewe ni nafuu, kwa vile unaponunua, hata anayekuuzia gharama zake ameingiza humo kwenye bei yake.
 
Nashukuru sana mkuu, umenirahisishia na kupata sehemu ya kuanzia.
Mungu akupe hekima zaidi.
 
2400 x 1100 =2, 640,000
Mkuu hapa tofali 2400 imara kabisa zinafika site Bila shida.
Hiyo 32800000 ni kwa sehemu gani dsm mkuu...

Hapo utakuwa umeokoa
Muda
Risk ya kuibiwa
Etc

Maelezo zaidi mkuu
 
Tofali nzuri tzs 1000 mpaka site. Ungetumia 2.4m. Ukifyatua mwenyewe usisahau gharama za muda wako au msimamizi na muda wa kusubiri hizo tofali vile vile maanake ukinunua leo unapata leo leo ila kufyatua ni siku kadhaa.

Mchanga lorry 8 kubwa 420,000/- ?
 
Vp mkuu, 420,000/- ni kidogo au kubwa. Tusaidie mawazo yako.
 
Mkuu ni wapi hapo unachajiwa sh 1000' garama ya tofali pamoja na kulisafirisha mpaka kwako. Na wanazingatia umbali wa kiasi gani?
 
mhh, huku kwetu tofali 1 ni elf 1 unafikishiwa mpaka site.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mashine ya aina gan
 
pia ujumlishe na gharama za maji ya kumwagia mpaka ziwe imara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…