Kulikoni mabasi ya Extra Luxury Coach?

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
198
Reaction score
209
Niliwahi kuandika juu ya jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kukamata basi la kampuni ya Extra Luxury Coach likiwa na shehena ya dawa za kulevya iana ya mirungi ikisafrishwa kutoka mkoani Arusha kwenda Jijini Dar es salaam mwaka 2023.

Basi hilo T643DVL, lilikamatwa eneo la majengo mapya wilaya ya Same baada ya askari wa usalama barabarani kulifanyia ukaguzi na kukutana na shehena hiyo, sijui polisi walimalizana vipi na wamiiliki wa basi hilo maana hatukuwahi kusikia tena habari zake,(soma habari hiyo hapo chini.

Kwa mara nyingine tena mabasi ya kampuni hiyo wamewasotesha abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Arusha kwenda Dar es salaam bila kuwapatia usafiri ndani ya wakati kwa mujibu wa taratibu baada ya basi lao kudaiwa kuharibika wilayani same mkoani Kilimanjaro .

Mkasa huo umewakumba abiria hao April 29 mwaka huu baada ya kukaa tangu saa moja jioni hadi kesho yake kwa maana ya April 30 kabla ya kufaulishwa kwenye basi la Kampuni ya Esther Luxury Coach.

Kabla ya mkasa huo, basi hilo lilikamatwa wilayani mwanga likidaiwa kusafrisha nyara za seikali lakini haijulikani jambo hilo liliishaje kutoka kwa maofisa wa maliasili na utalii waliofika eneo hilo na kufanya upekuzi kwenye basi hilo na kisha mzigo huo kuruhusiwa kuendelea na safari.

Mbali na hilo,abiria hao wanadaiwa kutozwa nauli ya sh,50,000 kutoka Arusha kwenda Dar es salaam kwa basi lenye choo ndani lakini matokeo yake wakapakizwa kwenye basi lisilokuwa na choo cha ndani,

Abiria mmoja alituma ujumbe kwa maofisa wa LATRA na hapa nautuma kama ulivyo.

"Hii basi ni ya kufungiwa,T791DXM ,tumekata tiket ya Luxury Bus yenye choo ndani na online inaonekana ni Extra Luxury Coach lakini si kweli,tumepakiwa kwenye basi halina choo,pia basi ilikuwa liondoke saa 12 lakini limechelewa sana kuondoka Arusha"

"Tumefika Himo tumekamatwa mpaka sasa basi limebeba nyara za serikali ,abiria tunateseka bila sababu ya msingi na tofauti ya basi la Luxury na ambalo si Luxury,pesa hatujarudishiwa,naomba hili ulifuatilie tafadhali"

"Tumefika Same basi tena limesimama,abira hatuna taarifa yoyote tumewekwq tu hapa".

"Mkuu hili basi abiria wamefaulishwa same muda huu ndo wanaondoka tangu jana saa moja jioni gari lilikwama Same na Trafiki naona wameliachia".

"Imagine abiria ambaye saa hizi alitakiwa kuwa amefika Dar ndo kwanza yupo Same",anamalizia abira huyo kwa kuhoji.

Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo aliyefahamika kwa jina la Massawe pamoja na kukiiri kutokea kwa mkasa huo anadai abiria waliendelea na safari baada ya kupatiwa usafri mwingine lakini pia akadai abiria walirejehsewa nauli zao kwa wale waliokata tiketi za sh,50,000 kwa basi lenye choo ndani .

SOMA HII YA MIRUNGI > Basi la Extra Luxury limekamatwa na mirungi 55kg
 

Attachments

  • EXTRA BUS.jpg
    74.9 KB · Views: 24
Mbona Kama wewe umetumwa kumchagua huyu Exra, maana kama ni mpandaji wa hili basi nadhani ungeshahama muda kutumia usafiri huu.

Sasa umekuja kusagia kunguni biashara ya watu,
Hebu wacha hizo maneno.
 

Disinformation Propaganda?
 
Umeandika kwa niaba ya Esther au Tilisho ?
 
Ndo maana mm naenda zangu na deluxe train polepole unalewa usiku mzima, kesho yake ukifka Moshi navuta bakuli la supu, chapati hawajui kupika walio wengi, nadandia shuttles huyo kijijini kwetu Tarakea. Ikiwa haraka sana dar express the best bus to i
 
Umeandika kwa niaba ya Esther au Tilisho ?
Muulize massawe wa Extra Luxury aliyemtafuta Esther Luxury coach siyo mimi na waliolalamika ni abiria soma vizuri walichoandika mangi acha kuwayawaya
 
Kikampuni kina vigari vitatu tu kikipata shida ndio shida yake hyo,hadi basi lingine liwafikie safari imeshakuwa kafir.
 
Punguza ujuaji
 
Bus zipo nyingi na abiria wapo wengi sana ila hii habari ipo kwa ajili ya kuchafuana na wanaofanya hivi ni wale Mawakala wao waliopigwa chini kwa hiyo wanatoa taarifa kwa vitu wanavyofanya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…