Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,258
Utafiti mpya uliotolewa nchini Marekani, umebainisha kuwa watu wanaopenda kulala bila nguo wanapata faida nyingi ikiwamo ya kuwa na uwezekano mdogo wa kupata ugonjwa wa kisukari.
Ripoti hiyo ya utafiti iliyotolewa na Taasisi ya Kitaifa ya Usingizi (NSF), inaeleza umuhimu wa watu kulala bila nguo kuwa ni kuimarisha uhusiano kwenye ndoa na kupunguza kalori nyingi.
Wataalamu wa usingizi wanasema kwamba ni vizuri mtu akawa katika hali ya utulivu wakati wa usiku kwa kuwa joto la mwili linahitaji kuteremka hadi nyuzi 50 za kipimo cha Fahrenheart ili mtu aweze kulala.
Wakati ubongo ukiendeshwa kwa ‘saa’ iliyo ndani ya mwili, hutuma ujumbe kuutaka moyo ufunguke au kufunga
“Joto la mwili huwa juu saa 5 usiku na kuwa chini saa 10 asubihi,” anasema Mkurugeni wa Edinburg Sleep Centre, ambaye pia ni mwandishi wa Kitabu cha Sound Asleep, Dk Chris Idzikowski.
“Kama kitu chochote kitazuia joto lisishuke, ubongo utahakikisha unajua kinachoendelea, hii inamaanisha, utahangaika kupata usingizi au utakuwa na usingizi wa mang’amunga’amu,” anasema mtaalamu huyo.
Ripoti hiyo inasema kuwa mtu anapolala bila nguo inakuwa rahisi kwa mwili kupoa na kuwezesha upatikanaji wa kiwango sahihi kinachohitajiwa na ubongo kufanya kazi.
Profesa Russell Foster, mtaalamu wa circadian neuroscience katika Chuo Kikuu cha Oxford, anathibitisha kuwa kulala bila nguo kunaboresha usingizi.
“Kama ulikuwa unavaa nguo nyingi za kulalalia, itakuwa vigumu kwako kupunguza joto. Kwa hiyo, punguza nguo unavyoweza,” anasema.
Anasema kuwa ikiwa usingizi umekatishwa kwa sababu ya joto kali, haimaanishi kwamba utapata usingizi mdogo wakati wote, bali unaweza kupata usingizi wa kushtuka shtuka.
Usingizi mzuri ndiyo unaofaa kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa kumbukumbu na uzalishaji wa homoni, kitendo ambacho ni muhimu kwa ukuaji wa seli na kuzifanyia marekebisho.
Kwa nini mwili unapoa wakati umelala?
Utafiti unasema kuwa siyo vizuri kuoga maji ya moto jioni wakati wa kwenda kulala, badala yake mtu anapaswa kupasha moto kigodo mikono na miguu yake. Hiyo ni kwa sababu ili joto la mwili lishuke hadi kufikia kiwango cha chini kinachochochea usingizi, mwili unatakiwa utoe jasho.
“Jambo hili linafanyika kwa kutuma damu kwenye mishipa karibu na ngozi- hasa kwenye mikono na miguu, ambako joto linapotea kwa njia ya ngozi,” inasema ripoti hiyo.
Hata hivyo, kama Profesa Foster alivyoeleza, kama mikono na miguu yako ni baridi, mishipa ya damu karibu na ngozi itapunguza kasi ya damu kutembea katika harakati za kutafuta joto na kuzuia lisipotee.
“Hii ina maanisha kuwa joto lako la kawaida haliwezi kushuka kirahisi,” inasema ripoti.
Taarifa hiyo inasema kwamba ndiyo maana watu wenye ugonjwa wa kuwa na mikono na miguu ya baridi sana (ugonjwa huo unawaathiri zaidi ya watu milioni 10 Uingereza, asilimia 10 wakiwa ni wanawake), ambao ndiyo wenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa kukosa usingizi, ‘insomnia’.
Hali hiyo husababisha mishipa ya damu kusinyaa, kupunguza kasi ya damu kutembea, kwa hiyo ingawa watu wanaosikia mikono yao ni ya baridi sana, joto lao huwa juu sana.
Ripoti hiyo inaendelea kufafanua kuwa wazee wana kawaida ya kujisikia baridi usiku, labla kwa sababu matatizo ya mzunguko wa damu kwao ni kawaida.
“Wanawake ndiyo wenye hatari zaidi ya kupatwa na matatizo ya baridi mikononi na miguuni, hasa wakati fulani wanapokuwa kwenye hedhi.
Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2008 na Taasisi ya Netherland inayojishughulisha na Sayansi ya Neva, pia unaeleza uhusiano wa joto la mwili na kulala.
Kuna baadhi ya watu walijitolea kuvaa nguo zinazozuia mabadiliko ya joto la mwili, ili kuwaruhusu watafiti kuchunguza joto kwenye ngozi bila kuathiri kiwango cha kawaida cha joto mwilini.
Timu ya watafiti hao waligundua kuwa wakati joto kwenye ngozi linapopanda kwa nyuzi 0.4, watu waliokuwa wanafanyiwa utafiti walikuwa na uwezekano mdogo wa kuamka wakati wa usiku. Lilipojitokeza kundi la wazee kufanya majaribio kama hayo, matokeo yalishangaza. Joto lilipofikia nyuzi 0.4, lilikaribia kuwa mara mbili ya hali ya kawaida ya kulala, pia lilipunguza uwezekano wa kuamka mapema kwa asilimia 50 hadi nne.
“Joto kwenye ngozi lilipoongezeka lilisababisha mirija ya damu kupanuka, hivyo joto kupotea kwa urahisi zaidi. Waliongeza uwezo wa kulala kwa kuongeza joto na kuruhusu kasi yake kutembea kutoka katikati ya mwili,” anasema Profesa Foster.
Kwa maneno mengine, ukitaka kulala kirahisi unahitaji kuwa na joto kali kiasi cha ambacho mishipa ya damu haiwezi kusinyaa, lakini siyo kuwa na joto kali mpaka mwili wako ukashindwa kupoa.
Namna ya kufanya
“Kuhakikisha kuwa joto lako la mwili linashuka vizuri, badala ya kuvaa soksi unapolala weka miguuni dumu la maji ya moto,” anasema Dk Idzikowski.
“Soksi haziruhusu joto kupungua miguuni, badala yake utaishia tu kuungua. Chupa ya maji ya moto inafanya miguu yako kuwa ya moto, lakini itapoa au unaweza kuondoa,” anasema.
Kisukari
Kwa mujibu wa utafiti kuhusu kisukari uliofanyika Marekani, wataalamu waligundua kuwa mtu akilala kwenye chumba chenye baridi anaweza kuongeza mafuta (brown fat) kwa watu wazima.
Vijana watano wenye afya nzuri walilala kwenye chumba chenye joto maalumu kwa miezi minne. Mwezi wa kwanza chumba kilikuwa na joto la nyuzi 24, baadaye lilishushwa hadi nyuzi 19, kisha likapandishwa hadi nyuzi 24 na mwezi wa mwisho ilipandishwa hadi nyuzi 27.
Vijana hao walikuwa wakila viwango sawa vya kalori na kuangalia namna insulini inavyofanya, kiasi gani kinahitajika ili kiwango cha sukari mwilini kiwe sawa, vyote vilikuwa vinapimwa kila siku.
Matokeo yalikuwa ya kushangaza. Baada ya wiki nne za kulala kwenye chumba chenye nyuzi joto 19, vijana hao walikuwa wameongeza mara mbili kiwango chao cha mafuta ya kahawia mwilini. Matokeo yalionyesha kuwa waliunguza kalori nyingi zaidi mchana wakati chumba chao cha kulala kilikuwa na baridi kali (ingawa si kiasi cha kupunguza uzito) na utendaji wa insulini nao uliimarika.
Mwandishi mkuu wa ripoti hiyo, Francesco Celi anasema kuwa utafiti umebainisha kuwa kutumia muda mrefu kulala kwenye chumba cha baridi kuwaweza kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari.
Profesa wa maendeleo ya saikolojia katika Chuo Kikuu cha Nattingham na mtaalamu wa mafuta ya kahawia, Michael Symonds, anasema kulala bila nguo kuna faida kubwa.
”Mafuta ya kahawia yanaweza kuzalisha joto mwilini mara 300 kuliko kuliko kiungo kingine chochote mwilini, inamaanisha kama ukiacha iendelee hivyo kwa muda mrefu ungeweza kupunguza nguvu ya ziada,” alisema.
Aliongeza: “Kwa hiyo chochote unachoweza kufanya kuchochea, kama vile kupunguza ‘thermostat’ na kulala kwenye baridi, linaweza kuwa jambo la faida sana.”
Hata hivyo, mtaalamu huyo anaonya kuwa joto kwenye chumba lisiwe chini ya kiwango ambalo hutajisikia huru, vinginevyo utashindwa kulala.
Anaendelea kusema kuwa watu wanaosikia joto kali usiku na wanapenda kulala bila nguo, wanaweza kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta ya kahawia, ambayo yanasababisha mtu ajisikie joto.
Chanzo: Mwananchi