Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,305
- 93,364
HEKIMA ZA TAIKON WA FASIHI.
Na, Robert Heriel.
Jumbe hii isomwe kwa lugha zao, kwa uelewa wao, kwa utashi wao, kwa mitazamo yao, nao wenye hekima wapate ufahamu. Lakini wapumbavu wapotee katika njia panda za fikara zao.
Niite Taikon wa Fasihi mwanafalsafa katika robo karne ya pili.
Kuishi ni akili. Maisha ni Akili. Bila akili hakuna maisha. Matokeo yanayotupata kwa sehemu kubwa ni sehemu ya maamuzi ya akili zetu.
Bila kujali matokeo hayo ni mema au mabaya. Kushindwa na kufaulu kwenye maisha hutegemea akili zetu. Hii ni kusema akili ni jambo nyeti linalohitaji kulindwa kwa nguvu zote.
Akili inatusaidia kuishi hivyo nasi twapaswa kuisaidia akili hiyo kuishi. Tukijua kuwa akili ni maisha. Akili ndio mtaji wa uhai wetu. Akili ndio jambo pekee baada ya uhai ambalo twapaswa kulipigania.
Tunajua akili huzaa uhai. Na uhai unalindwa na akili. Bila uhai hakuna akili, na bila akili uhai haudumu.
Mimi Taikon, kijana mdogo ninayeelea katika mwanzo wa pili wa robo karne. Ninayaandika haya kwa wenye hekima ili wapate kujua. Basi wenye uhai wanisikilize, lakini walio na akili watanifuata na kujua iwapasavyo kufanya.
Uhai unachanzo chake lakini pasipo akili twawezaje kukijua chanzo hiko. Uhai unapimwa na wakati naam ndio muda. Muda unaenda nao haurudi kwa waliowajinga.
Muda haurudi kwa mtu mpumbavu kwa maana hana akili ya kuurudisha muda huo. Lakini muda hurudi kwa mtu mwenye akili. Kwa maana anaakili ya kuurudisha muda huo. Ninafahamu ujinga hupendwa kwa sababu unamzaha.
Ninafahamu upumbavu una wafuasi wengi kwa kuwa umerembwa kwa nje nao kwa ndani ni mchafu. Hata hivyo wenye hekima hutambua na kuupuuza.
Akili inamilango saba walakini uhai una milango miwili. Wakuingilia na wakutokea. Kuingia ni nasibu ya akili na kutoka ni ukosefu wa akili.
Maisha bila akili hayadumu lakini akili ikiwepo basi maisha lazima yadumu. Kwenye akili kuna umilele wa kuwapo. Lakini pasipo akili kuna umilele wa kutokuwapo.
Adui ni yule anayeharibu akili. Wala sio yule akunyimaye chakula. Au akusemaye mabaya. Au yule akuumizaye kwa maumivu. Adui mbaya ni yule anayeharibu uwezo wako wa kufikiri.
Mtu anayekuharibu akili anataka akuue usiendelee kuishi. Utoweke usionekane tena hata katika kutokuonekana.
Nisemapo kuishi namaanisha kudumu milele hata ujapoondoka katika mlango wa pili wa uhai.
Akuuaye akili hutaka wewe uwe mtumwa wake. Umtumikie. Usiwe huru. Umtukuze yeye pekee yake wala usijitambue. Anataka umuone yeye ni bora kuliko wewe mwenyewe.
Mtu akiiua akili yako uhai wako upo mashakani. Kwa maana kuishi ni akili na pasipo akili hakuna maisha. Akiharibu akili utamuomba yeye chakula kijaze tumbo lako na ufahamu wako.
Akiiua akili yako utaabudu kile anachokiamini hata kama ni kibaya. Akikuua akili yako afya yako ndio huo uhai wako upo chini yake. Ni nini utafanya kwenye maisha pasipo akili? Kama kuna mwenye hekima aje kumjibu Taikon.
Usitafute mtu mwenye chakula ili akupe chakula ili upate mlo ambao kesho yake utataka tena. Mlo ambao ni ule aupendao huyo mwenye chakula wala sio wewe. Tafuta mwenye akili ili akupe akili ambayo itakusaidia kupata chakula ukipendacho.
Usitafute mwenye pesa ili akupe pesa. wala usitafute tajiri ili akupe utajiri. Usije baada ya kupewa baada ya muda ukaishiwa ukarudi tena kwa tajiri ili akupe tena.
Tafuta mwenye akili ili akupe akili za kupata utajiri. Akili mtu hupewa mara moja wala sio mara mbili kama vile ilivyo kwa uhai ambao mtu hupewa mara moja wala sio mara mbili.
Akili ni furaha kwa maana furaha haina matarajio. Furaha ni matokeo mshtuko wa hisia kwa jambo jema. Furaha haina matarajio. Furaha yenye matarajio sio furaha.
Na mara nyingi haidumu. Halikadhalika na huzuni. Huzuni haina matarajio. Ukitarajia kuhuzunishwa tayari hiyo yenyewe ni huzuni wala hutahuzunika siku utakapohuzunishwa kwa maana matarajio ndio huzuni yenyewe.
Ukitarajia jambo jema jua unatengeneza mazingira ya huzuni ikiwa jambo hilo halitatokea. Lakini usipotarajia jambo jema hata kama unalotaka basi unajitengenezea furaha ya kudumu.
Imani ni akili pasipo kuona kwa macho. Ndio maana nilisema Akili inamilango saba. Kuna tofauti kati ya Imani na matarajio. Imani ni uhakika kwa jambo ambalo halipo kwa sasa lakini unaliona litatokea.
Matarajio ni kuliona jambo lakini bila ya kuwa na uhakika. Ndio maana wenye imani wana furaha lakini wenye matarajio mara nyingi huhuzunika.
Mwenye haki ataishi kwa Imani. Yaani ataishi kwa akili. Naam ndio kuona pasipo kuona ambao ni moja ya milango ya akili.
Naweza kuwa naongea mambo ya kitoto yenye akili nyepesi ikiwa ni hivyo basi ngoja ni badili mfumo wa kuwasilisha.
Akili ni maisha. Akili hudumu. Akili ndio huleta furaha kwenye mizunguko yetu. Ndio! Katika mizunguko ya kila siku akili hutusaidia kuishi kwa furaha na amani.
Lakini Taikon, umeeleza mambo kadhaa hapo. Iweje usieleze chanzo cha akili?
Ningesahau lakini sio kwa makusudi kueleza asili ya Akili kutokana na kuwa swali hili nimeshalijibu. Umelijibu? Ndio nimelijibu.
Nilisema Hakuna akili bila uhai. Lakini uhai hauwezi kudumu pasipo na akili. Umekumbuka sasa yakuwa nilisema hivi? Anyway! Huenda naeleza kwa akili ndogo kiasi kwamba wenye akili kubwa mnashindwa kunielewa.
Uhai ndio kila kitu. Kila ukionacho kina uhai. Kwa maana uhai ni kila kitu. Lakini akili ndio inaendeleza uhai wa kitu au kukifanya kitu hicho kife. Hii ni kusema kama akili isipotumika kifu fulani huwe kufa. Lakini kifo ni matumizi ya chini kabisa ya akili. Yaani pale akili inapofika sifuri basi kitu au kiumbe hufa.
Hii haimaanishi kitu kilichokufa hakiwezi kuwa hai endapo akili ikitumika hata kwa nyuzi moja. Akili huleta uhai hata kwa kitu kilichokufa. Kwa maana vitu vyote havikuwa hai lakini vilipata uhai baada ya akili kutumika. Na pia vitu hivyo vilikufa kutokana na kutotumika kwa akili.
Bila shaka nimekujibu.
Usioe au kuolewa na mtu asiye na akili. Kumbuka kuishi ni akili. Na kwenye ndoa unaenda kuishi maisha ya ndoa. Kama ndoa mmoja wapo hana akili ndoa hiyo haitadumu. Itakufa tuu!
Mwenye akili huwa na sababu nyingi za kuishi ndoani. Lakini asiye na akili sababu moja tuu huweza kumuondoa ndoani. Mwanaume mwenye akili hafuati uzuri wa mwanamke bali humfuata mwanamke mwema ili amfanye awe mzuri na mwenye kuvutia hata kama mwanamke huyo alikuwa anaonekana mbaya yaani havutii.
Lakini mwanaume asiye na akili humtafuta mwanamke mzuri ili auharibu uzuri wa mwanamke huyo kisha humuacha.
Akili sio kuacha mke au mume wako. Akili ni kumfanya mumeo au mkeo kuwa bora. Kama alikuwa havutii mfanye avutie. Kama alikuwa haheshimiki wewe ndio unapaswa umfanye aheshimike. Hakuna mwenye akili akadharaulika.
Bila akili huwezi fanya biashara. Lazima itakufa tuu. Akili haina visingizio vya kushindwa kwenye jambo lolote lile.
Ukiona mtu anasingizia jambo lolote lile kuwa ndio sababu ya kushindwa kwake ujue mtu huyo ni mjinga.
Sababu ya kushindwa ni moja tuu, kuzidiwa akili na jambo husika yaani akili ilikuwa ndogo wakati unafanya jambo hilo.
Huwezi kufanya kazi bila akili. Kazi hiyo itakufa tuu wala haitadumu. Usishangae mtu anakuja ofisini kwako umhudumie wewe unatumia maneno machafu yasiyo na akili, ofisi ipo hovyo hovyo kama ofisi ya mtu asiye na akili, uaminifu sifuri hufuati muda wa ahadi.
Kumbuka akili ni uhai na uhai ni muda. Muda unadumu kwa mwenye akili lakini haudumu kwa asiye na akili.
Taikon niongee kwa kifupi na kwa njia ya wazi sasa. Akili ni Mungu, na kumcha Bwana ndio chanzo cha akili naam ndio maarifa.
Kuiheshimu akili ni kupata akili. Kuitafuta akili ni kumpata Mungu ambaye ndio uhai. Uhai haudumu pasipo na akili. Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa.
Bila kumcha Bwana kamwe huwezi kuwa na akili. Kama humchi Bwana ni wazi wewe huna akili kumaanisha hautadumu. Utakufa machoni na rohoni.
Basi na nipumzike sasa kwa maana yeye mwenye akili huhitaji mapumziko kwa ajili ya kustarehe akitafakari ukuu wa yule aliye mkuu.
Niite:
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Mwanafalsafa katika mianzo ya robo karne ya pili
0693322300 au 0711345431.