Idadi ya siku za kuingia hedhi imetofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine, kulingana na mfumo wa vichocheo wa kila mwanamke. Kwa walio wengi, hupata hedhi kwa kipindi cha siku tatu, nne na wengine hata siku tano. Lakini hedhi inayopitiliza zaidi ya kipindi hiki inaashiria tatizo la kiafya ambalo mwanamke hapaswi kulifumbia macho.
Ni muhimu kumuona daktari haraka ikiwa mwanamke anapitia hali hiyo na kupatiwa tiba stahiki. Sababu zinazochangia hedhi kupitiliza ni nyingi, likiwamo tatizo la kiafya linaloathiri utendaji kazi wa mayai ya uzazi linalojulikana kama
polycystic ovary syndrome (PCOS). Tatizo hili linasababisha kuyumba kwa mzunguko wa hedhi kati ya mwezi mmoja na mwingine, na hedhi inapokuja inakuwa ni ya muda mrefu kuliko kawaida.
Lakini pia maambukizi kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke, mathalani kwenye mfuko wa uzazi, kwenye mirija ya uzazi na hata maambukizi kwenye mayai ya uzazi, nayo yanasababisha hedhi kupita kiasi. Hedhi iliyopitiliza pia inaweza kusababishwa na uvimbe kwenye mfuko wa uzazi. Uvimbe huo hauashiria saratani, lakini ukiwa mkubwa unasababisha hedhi iliyozidi kawaida.
Baadhi ya njia zinazotumika kwenye uzazi wa mpango pia zinachangia kwa kiasi kikubwa hedhi kupitiliza...
NB:
Litro 👩