Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,718
Wanabodi
Hii ni Makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la Leo
Ili Kupata Majaji Watenda Haki, Tuachane na Majaji wa Hisani, Majaji Akiwemo Jaji Mkuu, Waombe Kazi, Wasailiwe, Wenye Uwezo Ndio Wateuliwe.
Declaration of Interest
Naomba kuanza kwa kutangaza maslahi, kuwa
Mimi licha ya kuwa ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea ambaye nafanya kazi kwa kujitolea kuelimisha umma kuhusu Katiba, Sheria, Haki na Wajibu, hivyo kila wakili ni ofisa wa mahakama, hivyo kufuatia majaji ni watu wanaoheshimiwa sana hadi kuitwa My Lord!, kitendo cha kushauri majaji hadi Jaji Mkuu waombe kazi, kisitafsiriwa kama ni dharau kuhusu uwezo wa waheshimiwa majaji wetu, ukweli kuhusu majaji wa hisani kwenye utoaji haki, uko wazi na bayana kabisa wala sio wa kumulika kwa tochi.
Nimeisha andika sana makala nyingi kwenye safu hii, kuhusu ukosenaji wa haki kwenye Mhimili mahakama, kuwa unachangiwa na uwepo wa baadhi ya mahakimu na Majaji, wenye uwezo mdogo wa kubaini haki, hivyo mtu anabambikiwa kesi, anabambikiwa ushahidi wa uongo, hakimu au jaji hana jicho la ndani la kuubaini uongo huo na matokeo yake an innocent victim anahukumiwa kwenda jela kwa kesi ya kubambikiwa kitu ambacho sio tuu ni dhulma na kinyume cha haki za msingi za binadamu, bali na pia ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu, mtu anapohukumiwa kifungo cha jela kwa kesi ya kubambikiwa, sio tuu, unamuathiri huyo mtuhumiwa pekee, bali unaiathiri familia yake, ndugu jamaa na marafiki na kuna wengine, mpaka anatoka, anakuta familia zimeisha paraganyika.
Hii inachangiwa na uwepo wa baadhi ya mahakimu na majaji waliopata vyeo hivyo kwa kuteuliwa tuu, lakini hawana uwezo na jicho la ndani lenye uwezo wa kubaini haki, majaji na mahakimu wenye jicho lenye uwezo wa kubaini haki, wakimwangalia tuu mtuhumiwa machon, kama mtuhumiwa huyo ni wa kesi ya kubambikiwa, jicho la ndani, litaona dhulma hiyo na sikio la ndani lenye uwezo wa kusikia sauti ya ndani, (The Voices From Within) litasikia sauti kuwa mtu huyu hana hatia, hii ni kesi ni kesi ya kubambikiwa, hivyo watamwachia huru mtuhumiwa na kuifutilia mbali hiyo kesi.
Mfano mzuri ni hii kesi inayoendelea sasa, (naomba nisiitaje, kuepuka kuingilia uhuru wa mahakama) ni uthibitisho wa wazi wa kesi za kubambikiwa!. Vijana wameandamana, wanapigwa kesi ya uhaini!, yule Binti Niffer, amesema tuu, neno “hakuna nywinywi, wala ninywi nywinwi”, kapigwa kesi ya uhaini!, kiukweli Watanzania Tumshuru sana Rais Samia, kumuelekeza DPP, kuzifuta kesi zote za kubambikiza.
Ili kupata majaji na mahakimu wenye uwezo na jicho la kubaini haki, inabidi nafasi zote za mahakimu na majaji hadi nafasi ya Jaji mkuu zitangazwe, Watanzania wenye sifa za waombe, wasailiwe, ndipo wateuliwe.
Kwa sasa majaji wanapendekezwa na tume ya utumishi wa mahakama, na kumpelekea rais majina ya kuteua, hawaombi kazi, wala hawasailiwi. Hii ilifuatia idadi ya wasomi wa sheria wenye sifa za kuwa majaji, walikuwa wachache, hivyo nafasi zingetangazwa, wasingepatikana, hivyo utaratibu wa kuteua ndio umekuwa ukifanyika, lakini kwa Tanzania ya sasa, tumefikia viwango vya kuwa na wanasheria wengi tuu wa kutosha, wenye sifa za ujaji, hivyo kunapotokea nafasi za ujaji, hadi Jaji Mkuu wa Tanzania, nafasi hizo zitangazwe kwa uwazi, Watanzania wenye sifa na vigezo waombe, wasailiwe, na katika usaili, kuwepo kitu kinachoitwa aptitude test, kubaini uwezo wa mhusika kubaini haki, wenye sifa ndio wachaguliwe na ndipo rais apelekewe majina ya kuwateua. Jirani zetu Kenya, wanafanya hivyo, hadi Jaji Mkuu anaomba kazi na anasailiwa.
Nimekumbushia hoja hii kufuatia kumsikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akizungumzia uwepo wa wafungwa magerezani waliofungwa kwa kesi za kubambikiwa, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TM)A) mkoani Dodoma.
Rais Samia amesema “Kesi nyingi zinakwama Mahakamani kutokana na kucheleweshwa kwa upelelezi au kwamba hazina ushahidi hizi tunaita kesi za kubambikizwa, nawapongeza Polisi kwa kuweka ukomo wa upelelezi kufikia miezi 6 kwa kesi ndogo na mwaka mmoja kwa kesi kubwa”.Rais Samia
Ameendelea kusema “Mahabusu kuna waliokaa wiki, mwezi,mwaka na kila anayeguswa upelelezi haujakamilika, nitoe wito kesi ambazo mna uhakika upelelezi hautokamilika basi watolewe wakafaidi uhuru wao, na zile kesi ambazo mna uhakika upelelezi utatimia basi uharakishwe” alimalizia Rais Samia
Rais Samia alisema Mahakama ni taasisi ya msingi katika ujenzi wa Taifa linalozingatia utawala wa sheria, haki, na maendeleo endelevu, na kusisitiza kuwa hakuna mfumo mbadala unaoweza kuchukua nafasi ya Mahakama huru na inayoaminika. Aidha, alibainisha uhuru wa Mahakama kuwa sharti la msingi la upatikanaji wa haki kwa wananchi na ni msingi wa imani ya umma kwa taasisi za dola, sambamba na kutoa rai ya
uwajibikaji, uadilifu, nidhamu na kuzingatia viapo vya kazi vya Mahakimu na Majaji.
Halikadhalika, aliwataka Majaji na Mahakimu kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ujasiri, akisisitiza kuwa imani ya wananchi kwa Mahakama ni rasilimali ya Taifa inayopaswa kulindwa na kuimarishwa kupitia vitendo na maamuzi ya haki.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Rejea

- Ili Mahakama Itende Haki: Mahakimu na Majaji waombe Kazi wasailiwe wenye Jicho la Haki ndio waajiriwe, Watazibaini kesi za Kubambikwa
- Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?
- Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?
- Haki, Haki, Haki! Serikali, Bunge na Mahakama hazina uwezo wala mamlaka ya kupora haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Je, jicho ona litaliona hili?
- Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of "Separation of Powers" Nothing, Just a Myth!
- Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?