Mnyakatari
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 2,113
- 1,926
PSG imeteleza baada ya kulazimishwa sare jana huku arsenal wakipanda juu kwa ushindi wake mnono dhidi ya Basel jana.Leo kuna mechi za kumaliza mzunguko wa makundi.
Kundi A PSG na Arsenal yeyote akiteleza anajikuta nafasi ya pili pale wanapokutana na timu zisizo na nafasi.Basel wanawakaribisha arsenal na Ludogorets ni wageni wa PSG.
Besiktas imegalagazwa na Dynamo kiev goli 6 bila.Kwa hiyo zote zimeaga huku Napoli na Benfica(ingawa walifungwa jana na napoli) zikifuzu raundi inayofuata.Kundi B Besiktas inahitaji ushindi wa lazima pale itakapokaribishwa na timu inayokamilisha ratiba Dynamo Kiev.Ushindi wowote kwa Besiktas utaihakikishia nafasi mbili za juu kwenye kundi.
Benfica inaikaribisha Napoli na kila timu itasaka ushindi hapa hasa Napoli ambayo inajua droo yoyote itaihakikishia nafasi Benfica huku yenyewe ikiombea Besiktas isipate ushindi.Ili kujiweka mbali na utegemezi wa matokeo ya mechi ya besiktas napoli wanahitaji ushindi.