Kosa wako utalia sana

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,193
^^
Dunia imeumbwa kwa ajili ya wawili,
Tena wawe mke na mume,wafarijiane katika raha na tabu.
Kosa wako,utalia sana
...
Utajifariji kuwa utasimama mwenyewe,nje uta tabasamu kwa furaha Lakini wakati utafika utahitaji mtu wa jinsia ya tofauti.
Mfarijiane na kuinuana
Kosa wako,utalia sana
...
Usiombe kukutana na wapenzi wapitaji,
Waletao furaha ya muda na kukuliwaza,
Wakakujaza amani kisha wakaondoka,asiwepo maalum kwa ajili yako
Kosa wako,utalia sana
...
Usiombe aliyestahili kuwa wako wa daima
Awe alishaitwa mbele ya haki bila we kujua,
Utaparamia miiba watu,waurarue moyo
Kosa wako,utalia sana
...
Ukiwaona wanandoa,
Wakipita njiani kwao,
Wakicheka na furaha,
Unaweza dhani hawana makovu ya mahusiano,ukikumbuka u mpweke
Kosa wako,utalia sana
...
Ukitazama gharama ya kumpata mpenzi,
Penzi linauzwa kwa pesa,na wenye pesa wanalitafuta hawalipati,na ukatazama viraka vya uchumi ulivobeba.
Kosa wako,utalia sana
...
Usiombe uwe na ndoa mkose sauti ya mtoto,
Mtoto aliye tokeo la muungano wenu wa haki,muwatazame wa jirani yenu tu!
Kosa wako,utalia sana
...
Dunia iuende gereza
Gereza la matajiri wa upendo lakini hawana wa kuwapenda aidha kwa mipango ya Mungu au maamuzi ya wanadamu!
Kosa wako,utalia sana
...
Heri usilie wala kulalamika,tena usiwaseme vibaya waliokuachia makovu,ukayasahau machozi,Ukamshukuru Mungu,hakika utalia,dunia haitosikia.
MAJONZI YAPO MOYONI
^^
 
Ubeti wa nne umenigusaa, nahisi aliyestahili kuwa wangu kashatangulia mbele za haki....ila ubeti wa mwisho wa muhimu zaidi, ameeen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…