Ni ukweli usiopingika kuwa tuna Wabunge wenzetu ambao ni Wanasiasa uchwara tulionao bungeni ambao nawaita ma-agent wa mafisadi waliotaka kusambaza mafuta feki na pia wale wenzao wanofisadi TANESCO kupitia mapato ya majenereta yao. Ni hawa ambao wanaoshangilia tuwapo gizani maana hiyo ndiyo mitaji yao. Wanaonekana kuhangaika sana kutokana na misimamo na uadilifu wa Watendaji wa sasa wa Wizara ya Nishati na Madini. Mbinu zozote wanazopanga za kuanzisha vurumai ndani ya Wizara hiyo zimeshindwa kwa jina la umoja!
Serikali itable hiyo sera ya gesi ijadiliwe na wadau wote husika; Wizara ikamilishe mpango wa upatikanaji na usambazaji wa gesi kwa ufanisi- Wananchi wa Mtwara na Watanzania wote kwa ujumla tunufaike.
Ili kuisimamia Serikali vyema na kusafisha uozo nje; tunatakiwa kuanza ndani ya Bunge kwa kuwachomoa hawa ma-agent wa mafisadi Bungeni. Tutawakaba kooni muendelee kuwa masalia!!!