Kuna motor ndogo ndani ya simu ndio inayosababisha vibration. Kinachotokea ni kwamba hiyo motor imetengenezwa kwamba haija balance yaani upande mmoja mzito kuliko mwingine kwa hiyo kunakuwa na mzunguko usio sawa ndio maana simu inatetemeka. Yaani ni kama vile tairi la gari lenye uvimbe upande mmoja litafanya gari kurukaruka. Motor hiyo ingelingana kungetokea mgurumo laini bila mtikisiko.