Kisasi Cha Mahaba.....

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230
Habari za usiku nyote,

Nimekutana na hiki kisa mahali na kwa chumvi niliyokula hapa duniani nimeshuhudia mahali mahali.

Hii ni habari ya kweli kabisa;

Mschana Nasra ni binti pekee kwenye familia yao, mpole mwenye heshima na adabu zote mtaratibu na mkimya. Aliyapenda masomo yake sana na kutia bidii shuleni.

Nasra alikuwa na kaka zake na wadogo zake wa kiume ambao walikuwa watu du kiasi. Kaka zake wakiwa shule ya sekondari mmoja wa kaka zake akatembea na mschana mmoja yule mschana alichanganyikiwa na mapenzi akashindwa shule. Sasa huyo mschana nae alikuwa na kaka zake baada ya kuona dada yao kaonjeshwa penzi na hao vijana wakasema na nyie si mna mdogo wenu wa kike? Wakaweka kisasi na ikawa kweli.

Kaka wa binti aliyeshindwa shule baada ya kuchanganyikiwana penzi la kaka yake Nasra, akaanza kumtaka urafiki Nasra akiwa form 3, nasra alizidiwa na maneno matamu pasi kujua penzi analotakwa nil a kulipa kisasi kwa kosa alilofanya kaka yake. Binti alishika mimba na hakumwambia mtu yeyote yule.

Nasra akajifungua pasi kufanya mtihani ya mwisho form 4 na shule ndo ikawa basi.

Hivi kwanini wewe binadamu ukifanyiwa ubaya na Karim, kwanini kama una nia ya kulipiza ubaya usiulipize kwa Karim mwenyewe badala yake uufanye kwa watoto wa Karim au wadogo zake au wazazi wake?

Ni hasira gani hiyo? Imeniuma sana binti mrembo hajamaliza form 4 saa hizi bado ananyonyesha na maisha ya kwao ni duni uwezo wa private school haupo.... yaani nyie binadamu..... kwanini lakini visasi?

Athari ni kubwa katika familia ya Nasra, baba na mama yake hawana maelewano kila mmoja akimtupia lawama mwenzie kwa kuwa kisababishi cha Nasra kupata mimba akiwa anasoma.


Wanaume punguzeni hasira za visasi vya mahaba ndo mnapelekea wadada wengi kuwa singo mazas halafu baadae mnaanza kuwananga oooh singo maza sio wa kuoa.......

Who made singo mazas? Have you get into their feet what they pass through? ?

Yaani hii habari imenihuzunisha sana, ni mmoja wa mabinti waliojitokeza leo kwa makonda.

Usiku mwema, mlio wahi kukomenti saa zingine muwe na subira kidogo sio kila kitu ni nyeegee.

Kasie Mambo Yote.
 
Kisasi ni kitu kibaya sana na huwa hakina mwisho kama wahusika wote wakiwa na roho hiyo,

Hapo utakuja kushangaa watt watakao zaliwa wanaendeleza hivyo visasi...

Hao jamaa waliompa mimba Nasra walipungukiwa akili na busara maana kumfanya mtu alipe makosa ya mtu mwingine tena bila kuhusika hata kidogo ni ujinga,

Nasra wa watu kakosa shule...mtoto atalelewa na nani!!?

Wavulana wana matatizo sana...ndio chanzo cha singo mazas.
 
Umeongea kwa uchunguuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…