Kisa cha bwana mmoja na nyoka

Chrysanthemum

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
1,972
Reaction score
7,144
Wanajamvi kuna kisa cha siku nyingi kuhusu Bwana mmoja na Nyoka.

Siku moja bwana mmoja alimwona nyoka aliyekua kanasa katika mzigo wa kuni uliokua ukiungua.

Pasipo kujali, Bwana yule alitia mkono wake, kumvuta nyoka yule kutoka moto ule wenye joto kali na miale. Mara ghafla nyoka yule aligeuza kichwa chake na kung'ata mkono wa yule bwana. Maumivu yalikua makali sana kitu kilichomfanya yule jamaa kumwachilia yule nyoka akaanguka katika moto ule.

Baada ya hapo yule bwana akachukua mti kwa Mara nyingine akijaribu kumwokoa yule nyoka. Baadaye Nyoka alisaidiwa na kutolewa katika moto na kuwekwa pembeni kisha akazamia katika mawe yaliyokua kando.

Kuna mpitanjia mmoja aliyekua akipita katika eneo lile hivyo alishuhidia kila kitu alishangaa sana akaamua kumuuliza yule Bwana..."Ni kwanini umeamua kumsaidia Nyoka huyu japokuwa alikung'ata ulipojaribu kumsaidia?"

Yule bwana alijibu "Najua ni asili na tabia ya Nyoka Kung'ata, na tabia hiyo haiwezi kubadilika na hiyo haiwezi kubadilisha asili yangu ambayo ni kupenda kusaidia wengine"

Usibadili asili yako, hata kama kuna watu wamekuumiza, wamekusaliti au wamekukatisha tamaa

Usipoteze utu wako kwa watu wengine, cha muhimu ni kuwa na tahadhari.

Ben Carson
 
doesn't apply in real life, bite me once and i will sever your head!
 
Last edited:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…