Kiribatumbo ni ongezeko la kiwango cha mafuta mwilini kilichozidi salama na kusababisha athari katika afya ya mwanadamu.
Mtu mwenye kiribatumbo ni yule ambae BMI ni zaidi ya 30.
BMI -Body Mass Index ni kipimo cha uwiano baina ya uzito wa mtu na urefu wa mtu.
BMI hutumika kuonyesha uzito wa mwili ulio salama na usio salama
Uzitouliozidi salama. BMI- 18.5-24.9
Uzito pungufu BMI- chini 18
uzito uliozidi salama BMI - 25-29.9
Kiribatumbo BMI zaidi ya 30
VISABABISHI
1- Ulaji wa vyakula vya mafuta ,wanga na sukari kwa wingi
2.Kukosa kufanya mazoezi
VISABABISHI KWA WATOTO
1. Sababu za kurithi hasa maumbile
2.Lishe isiobora kwa mtoto hasa pale ambapo mtoto anakosa maziwa ya mama na kula vyakula vya viwandani katika umri mdogo
3. Tabia ya mzazi kutomruhusu mtoto kushiriki mazoezi au michezo ya kitoto
4. Mtoto kutumia masaa mengi kuangalia tv au kucheza game
5 . Ulaji wa vyakula vyenye mafuta ,sukari au vya viwandani kwa wingi mfano chokolate ,pipi,sosaji,chipsi ,mayai, na majuisi au soda kwa wingi.
DALILI NA ISHARA ZAKE
1. uzito wa mwili usio kawaida
2. kutanuka sehemu mbali mbaliza mwili mfano mikono,mashavu,tumbo na mapaja au miguu
3. Nyama uzembe/mafuta sehemu tajwa hapo juu
4. Kuchoka choka pale mtu anapofanya shughuli ndogo
5.Matatizo ya moyo na kisukari
WAHUSIKA IDADI ZAO
Tatizo hili huwapata watu wa rika lote
kutokana na lipoti ya WHO 2016
watoto chini ya umri wa miaka 5 takribani 41 millioni duniani wanauzito uliozidi salama au kiribatumbo na zaidi ya asilimia 50 wanatoka nchi za Africa hasa zenye uchumi wa chini na wa kati
kati ya miaka 5-19 takribani millioni 340 duniani
Watu wazima zaidi ya umri wa miaka 18 wenye uzito uliozidi salama au kiribatumbo wanakadiriwa kufikia billioni 1.9 duniani
ATHARI ZA KIRIBATUMBO
1. Magonjwa ya Moyo
2. Ugonjwa wa sukari
3.Cancer ya kizazi,matiti
4. Kuvunjika mifupa kwa urahisi
5.Matatizo ya viungo vya mwili
ATHARI KWA MTOTO
1.kisukari cha utotoni
2.dalili za awali za magonjwa ya moyo
3.kuchelewa ukuaji
4.mtoto kujitenga na wenzie kutokana na kujiona tofauti
5. Unyanyapaaji
MBINU ZA KUJIKINGA
1.Kupunguza vyakula vya mafuta ,sukari na wanga
kula kiasi cha wastani kwa matumizi ya kila siku.
Hakikisha kiwango cha chakula unachokula kila siku kinaendana na shughuli zako
Punguza au acha matumizi ya vyakula vya viwandani vyenye sukari ,chumvi yakuongezwa iliyozidi kawaida.
2. Fanya mazoezi kila siku
kwa watoto apate muda wa michezo kama sehemu ya mazoezi walau dakika 60 kila siku
Kwa mtu mzima afanye mazoezi kila siku muda usiopungua dakika 30 na atoke jasho la kutosha
Fanya zoezi kwa malengo husaidia kutokata tamaa na kuishia njiani
3. Punguza matumizi ya vyombo vya usafiri kwa umbali mdogo au wa wastani.
kutembea mara kwa mara husaidia kupunguza mafuta mwilini
kwa ushauri nitafute 0718 22 48 40
#ptjosephmwanangwa
#elimufiziotherapia #elimukwajamii #physiotherapyclinicununio #physiotherapyTanzania #physioplusdar #obesity#kiribatumbo#BMI