Kipimo Cha moyo

Kipimo Cha kucheki tatizo kama moyo uko na shida
Kuna vifaa tofauti vya kupimia moyo, lakini kitu muhimu sio tu kupima bali kujua kusoma matokeo.
Na unatakiwa kupima ukiwa umetulia kwa muda kabla ya kupima
Cha kwanza na nadhani ni rahisi kupata hapa bongo ni kipimo cha msongo wa damu, hiki kitaonyesha kama mapigo yako ya moyo yanafanya kazi ya kusukuma damu mwili katika hali ya afya salama ya moyo.

Majibu yanayoonyeshwa ni majibu mawili ya Systolic yaani nguvu ya moyo kusukuma damu kwenye mishipa(Namba kubwa) na Diastolic yaani nguvu wa damu wakati moyo uko kwenye mapumziko kati ya kila msukumo(Namba ndogo)
Hivi ni vishiria vya kama pressure kama tunavyosema iko juu au iko chini
Majibu ya 120 -130 (Kubwa)/80-90 (Ndogo), mapigo yako salama na moyo unafanya kazi vizuri.
Majibu ya Kuanzia 140/100, na kwenda juu hapo ndo wanasema una pressure kubwa na unatakiwa kumuona daktari wa moyo, sio vilaza wa dispensari.

Na vipimo vikionyesha 90/60, sio mbaya kama ni mwana michezo au ni mu wa mazoezi, lakini kama sivyo haya majibi yanaweza kufanya unasikia kizunguzungu na kujisikia umechoka sana
Angalia hapa viwango vya vipimo na maelezo yako ambayo nadhani utayaelewa baada ya ufafanuzi niliotoa


Siku hiz kuna saa janja hasa Apple, Samsung na Huwaei zinapima moyo kwa ustadi mkubwa ila ndio bei zake sasa, lakini sikushauri ununue za kichina bora ununue hiko kifaa nilichoweka hapo juu.

Kuna vifaa tofauti kama ECG ila hii ni ya kitaalamu zaidi na unashauriwa ifanyike hospitali tu au Heart Rate monitor ambazo hata saa janja nyingi zinakuwa nazo lakini majibu yake sio ya kuamini
 
Nataka kujua gharama za matibabu ya hospital Mkuu?
 
Vipimo vya,moyo vipo vingi, inategemea nini kinapimwa;
1. Electrocardiogram (ECG)
2. CT scanner
3. Echocardiogram
4. Machine za kuvaa mda mrefu ili kupima mwenendo wa moyo, 24hrs hadi 30days
Bei inategemea nini kinapimwa, kifaa gani kinatumika na ukubwa wa tatizo.
Una shida ya moyo Bushmamy au ni mtu wako?
 
Nahisi siko sawa kifuani , nahitaji kucheki mkuu
Pole sana mkuu, nenda hospital. Kila kitu utajua huko huko, usisubiri maana tatizo likiwa kubwa matibabu pia ni changamoto.

Pole mkuu, kama upo Dar nenda tu hapo Jakaya. Japo kimsingi matibabu ya moyo kama huna bima yapo juu, kwa kuanzia naamini wataanza na ECG ambayo sio ghali sana.
 
Maumivu chini ya kifua upande wa kushoto, kizungu zungu kikali
ECG
Echo
BP
Full blood pictures
Chest x Ray

Kwenye 200k hiv


Sio lazima iwe ni matatizo ya moyo inawezekana
pia kuwa ni gesi kujaa kutumboni , shida yake inaweza pelekea ukafikiri ni matatizo ya moyo , ukienda hospital utapata uhakika zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…