Daah! Nakumbuka Kuna siku moja mitaa ya uhindini mjini Dom hio daah! Nko na mwanangu mmoja sangu now marehemu tumeambatana na dogo mmoja hv anaitwa nata, tukaenda nyumba ya dingi moja hv liliwahi kua kuu la wilaya huko iringa lilikua refu afu KUBWA liko so powerful, lengo letu lilikua kuiba mapera maana yule dingi alikua anakaa peke yake Hana familia nyumba yake ilikua karibu na tbc Kanda ya Kati pale uhindini, mapera mekundu kinyaaama! Nyumba Ina fence ya michongoma! Ce tukazunguka pembeni ya nyumba yake kulikua na pagale, tukaanza tungua mapera, Sasa Mimi tamaa zangu zikaniponza, baada nichume mapera ya karibu c nikafata Yale ya mbali, nikawa nimeingia ndani ya nyumba ya yule mzee ingawa Niko juu ya mti, yule mzee akasikia kukurakakara zile akafurumuka ndani, mwenzangu mmoja akajificha pagaleni mwingine fasta akakimbia mie ile natua tuu dingi hili hapaaa! Limebeba mbao ngumu mkononi! Nikadesh nilipige chenga nkafanikiwa Sasa ile naruka mtaro likarusha mguu nikaenda chini!!!! Daaaah! Aisee Lile dingi lilinipiga Kama linaua nyoka!!! Lilinitandikaa mamaeeee!nilivimbaa mikono, miguu! Nikafanikiwa kuinuka ila nshaivisha vibaya nachechemeaa! Eti hasira za kitoto nlivofika mbele acha nianze kumporomoshea matusiii!!!