Nadahani siyo sawa, Ngassa au Tegete bado wadogo tu kwa umri likely 23yrs. Ngassa alikosa Westham kwasababu ya mabavu (nguvu) kitu ambacho si shida kwa Wenger, pia dogo atakuwa ameshajiweka sawa baada ya kuikosa Westham. Ngassa, Kig, Tegete na Mgosi ni wachezaji wazuri sana. I hope Wenger na makocha wengine watawaangalia hawa madogo.
tuendelee kuzalisha wengine, akina Bunu (kama sikose) yule kinda aliyeibukia coca cola ya vijana akaenda Brazil.
Wasiwasi; kuondoka kwa Maximo kunaweza kudidimiza soka letu, hawa wazungu (Paulsen) si wavumilivu. Mpira wetu, utaratibu wa TFF na Serikali kwa ujumla unahitaji kocha anayejitolea kwa moyo mkuu.