Nyanya ni zao la mboga linalolimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara.
Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani.
Kwa Tanzania, nyanya ni zao la kwanza katika mazao ya mboga linalolimwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha na mboga zingine.
Nyanya hutumika karibu katika kila mlo.
Kulingana na umuhimu wa zao hili kama chakula na pia kama zao linalomwingizia kipato mkulima, kuna haja ya kutoa mafunzo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wake.
Soko unapaswa kulitengeneza mwenyewe kaka. Mimi nilikuwa nawaza kama wewe kwa upande wa Mishumaa, nikasema sipaswi kusubiri fulani nisiyemjua aje kunihakikishia soko. Nikaamua kulitengeneza mwenyewe, sasa nina wateja wa uhakika