Kilichopo Zanzibar hivi sasa ni UZANZIBARI kwanza au niseme Zanzibar kwanza halafu Tanzania au Muungano.
Ikiwa kuna tishio huko Mombasa kuwa hawatapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao wa Kenya kwa sababu Mombasa si sehemu ya Kenya kutokana na nyaraka za zamani ,tunaweza kusema Mombasa ni sehemu ya Zanzibar na hivyo kuwa ni sehemu ya Tanzania kwa sababu za Muungano.
Kwa WaZanzibari ,wao wapo na nchi yao na katika jambo lolote lile wanahakikisha Zanziabar inakuwepo na kubakia kama Zanzibar na serikali yake,Raisi wake ,na kila kitu kimamlaka inabakia nchi kamili na kuhakikisha inarudi katika UN.
Je ni nchi gani ina ofisi mbili za UN ,kisheria hakuna ,inakuwaje Tanzania bara (Tanganyika) kuna ofisi ya UN na Zanzibar kuna ofisi ya UN ? Hivyo tunakokwenda ni kuwa kila mmoja kuwa na nchi yake ,Tanganyika kwao na Zanzibar kwao na hili halitaki kuwepo na ugonvi wala chuki bali kama tulivyoungana kwa furaha na bashasha ndivyo hivyo hivyo tutakapohitimisha kwa hayohayo ya furaha na amani kabisa. Yote ni hiyo KATIBA IJAYO.
Sasa tatizo ni huko Tanganyika ,kwani kama tatizo litatokea katika KATIBA mpya na kukosa utatuzi itamaanisha ndio mwisho wa Muungano.
Je Tanganyika kutakuwa salama ? Jawabu kwa watanganyika wengi wanahoji na huko Zanzibar kutakuwa na amani ?
Hali ilivyo kwa Zanziabar bila ya shaka yeyote ile amani itakuwepo na ndio hii ambayo inaendelea kuundwa kwa kuwekwa na kurekebishwa kwa Katiba ya Zanzibar ,bomu linalochemka ni huku Tanganyika ambako KATIBA iliyopo imekaa kimuungano na nchi nyingine.
WaTanganyika wamejitayarisha vipi ikiwa Muungano utavunjika ? Kwani serikali iliyopo ni ya Muungano ,haiwezekani ikaendelea kuwepo ikiwa Muungano haupo. Nionavyo kuna umuhimu wa kuunda serikali ya Tanganyika .
Hapo Mombasa kuda data zinazoonyesha Mombasa ilitolewa kwa mkataba wa miaka mia na mahesabu yanaonyesha imeshatimia ,aidha Tanzania au Zanzibar ukichanganya na wazalendo wa Mombasa ndio wenye mpini kuliko serikali ya Kenya ,Kimataifa(UN).Goma hiloooo,,,, hehehee!! Wa "tanzania bara" wanakazi kweli kweli, na apo ulipogusa kuwa mombasa wanataka kugoma kupiga kura wakitaka wawe chini ya dola ya zanzibar mbona ni habari yamshtuko?!! 😀 kaaaazi kweli kweli,,, ila kwa nnavyojua mimi kuwa mfalme alizituoa/kuziuza izo sehemu za mombasa, Lamu na nyenginezo, mana wakisema ivo basi kanda ya pwani yote ya tz bara ni ya zanzibar,,, jeee patatosha apo?!!