Kikwete hakukosea kwa Wassira

mtahengerwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2011
Posts
384
Reaction score
173
Mabadiliko aliyofanya Rais Jakaya Kikwete ya kumhamisha mhe. Wassira kwenda wizara ya kilimo chakula na ushirika ni uamuzi sahihi kwani wizara hii inahitaji mtu mwenye kuguswa na maisha halisi ya watanzania ambao wengi wao ni wakulima.

Tumekuwa mashuhuda wa jambo hii kwani kila waziri akipelekwa wizara hiyo hupwaya! Mfano halisi ni prof. Magembe na eng. Chiza, hawa wote badala ya kutatua matatizo ya makulima wao hutengeneza matatizo.

Sasa ni Mara ya tatu kwa mhe. Wassira kuwa katika wizara hiyo kwa kipindi cha uongozi wa Kikwete, hii ina maana kuwa waziri pekee mwenye suluhisho ya matatizo ya watanzania ni Wassira ndio maana kila siku rais anahangaika kumbadilisha na kumpeleka wizara zenye matatizo akatatue na kupambana na changamoto za wizara hizo.

HONGERA SANA WASSIRA!
 
Pamoja na mengine lakini pia kapelekwa huko ili kumnusuru asifukuzwe kwenye nyumba ya bodi ya sukari ambayo tayari alishaamriwa aihame. Sasa naona kamwambia JK amrudishe huko ili aendelee kukaa kwenye nyumba hiyo iliyoko Masaki jijini Dar es Salaam.
 

Poleni sana Lumumba! hamna bahati kwani hamuwezi kwepa adhabu ya Mungu
 
Wassira simkubali kwa lolote..... gamba chakavu!!!
 

Wasira nilini aliguswa na matatizo ya wanachi?
 
Jamani mimi binafsi baada ya kusikia scandal ya nyumba inayolalamikiwa ilibidi niende kuiona na baada ya kuiona nikaangalia na nyumba zungine za mawaziri, ni WASSIRA pekee anayeishi kwenye nyumba mbaya kuliko viongozi wa hadhi yake.Kitu kinachonishangaza pamoja na kuishi kwenye gofu hilo hajawahi kallaamika isipokuwa kamati ya PAC.Hata mimi naungana na PAC kwamba aondolewe kwenye gofu hilo na kutafutiwa nyumba yenye hadhi ya kukaa waziri wa kilimo chakula na ushirika
 

Nikupe pole mtoa mada.badala ya kuhuzunika unatoa pongezi mimi nikiwa mwanachama hai wa ccm inatakiwa tujiulize kwa nini kocha anabadili wachezaji kila mara na bado timu yetu inafungwa atujiulizi kuhusu hilo bali tunang'ang'ania kupongeza tuamke tumwambie kocha hii inatosha wewe ndio mwenye matatizo kaa pembeni tunaweka mwingine tuache unafiki tuwe wakweli wana ccm.sasa hivi tumeanzisha bajeti zisizo rasimi angalia mfano hai kwenye picha hizi
 

Attachments

  • 1422370411284.jpg
    55 KB · Views: 243
  • 1422370426203.jpg
    63.8 KB · Views: 234
  • 1422370441691.jpg
    99.3 KB · Views: 147
  • 1422370455190.jpg
    83.3 KB · Views: 146
Hata kama kocha ni mubovu lazima ahangaike timu yake isifungwe hivyo hujitahidi kuweka wachezaji ili kuzuia asiendelee kufungwa au anatumaini anaweza kufunga .ukiona kocha ni mubovu then hataki kufanya mabadiliko huyo hafai
 
Wassira na Anna Kilango hawakuwa na fadhila nyingine toka kwa rais muda huu iliobaki kwa sababu walikuwa msaada mkubwa kwa rais,chama,kumaliza malumbano makali yaliyotaka kuingiza nchi kwenye matatizo makubwa.ikumbukwe watu Hawa wawili walifanya kazi kubwa sana ktk kamati iliyoundwa na spika Maki da kutafuta suluhu kibunge siku ambayo wabunge wa upinzani walipotaka kutoka nje baada ya wabunge wa Ccm kutetea wizi wa Escrow.watu hawa waliwaongoza wabunge wa Ccm mwenye kamati.nitashindwa kuieleza vizuri ila utakuwa umepata picha.
 
Nyoko zenu, kama alilijua hilo kwann asingemuweka toka mwanzo? Wote nyie ni wezi tuu!! Mtaweweseka sana mwaka huu hii ndo ungwe yenu ya mwisho!!
 
Teeehteeeeh
Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Ni Shedeeeedaaaaaaaaa,
walimuita Jaji Warioba kuwa ni shida sasa wao ndio wamekuwa mara mbili yakeee.
 
Mh.tuna shida ya maji tangu uhuru mpaka sasa,hii shida itaisha lini?hili Swali aliulizwa Wassira na wananchi wa jimboni kwake!jibu_mnaniuliza maji mimi mvua?kwa jibu hili hatakiwi kupewa wizara yyte ile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…