Kikosi bora cha timu ya Mpira wa Miguu cha England kuwahi kutokea

Wangapi mnakikumbuka Kikosi hiki kilichoshiriki Euro 96 palepale kwao England
Umenikumbusha Paul Gascoine " Gazza " aliyeavaa jezi namba 8, moja kati ya Viungo bora kabisa wa Kiingereza, katika ubora wake alikuwa moto wa kuotea mbali sana.

Licha ya Kipaji Maridhawa alichobarikiwa na Muumba ila matumizi makubwa ya Pombe yalimfanya ashindwe kutamba sana uwanjani.

Pia nimemkumbuka Alan Shearer, Straika hatari wa Kiingereza, mpaka leo ana magoli 260 katika EPL ndio mfungaji bora wa wakati wote wa EPL. Na yeye pamoja na Kipaji kikubwa cha kutupia, alimkatalia Sir Alex Ferguson mara mbili kwenda Man Utd.
Ya kwanza wakati anatoka Southampton kwenda Blackburn.
Mara ya pili aliikataa Man Utd wakati anatoka Blackburn kwenda Newcastle Utd.
Unahitaji ujasiri wa hali ya juu kumkatalia Meneja Mahiri kama Sir Alex.

Mtoa mada naomba utuletee Kikosi cha Blackburn Rovers kilichotwaa ubingwa wa EPL katika siku ya mwisho ya Msimu wa 1994/1995.

Mpira sasa umebaki kwenye mbinu za kujilinda kuliko burudani.

Ahsante mtoa mada.
 
Gazza nakumbuka kabla ya kwenda kupiga mkwaju wake wa penalty alikuwa akiongea na baadhi ya wachezaji wa jeremani ilikuwa kama anawaambia mimi nikienda pale nawafunga tu na alipiga penalty nzuri tu jamaa waqt yupo lazio kuna siku kamuokota nyoka akamuwekea di matteo mfukoni siku nyingine kocha wao dino zoff kamkwapua filimbi kisha akaenda kumfungia ndege (bird )aliporuka akasepa nayo. Kuhusu Blackburn rovers hicho kikosi shy given na Tim flower ndio walikuwa walinda mlango huko mbele alikuwapo Chris sutton watu kama hanning berg hata gremie le saux pia alijumuishwa kikosini.
 
bila kumsahau Nahodha Tim Sherwood. Kocha akiwa King Kenny Daglish
 
Nakumbuka nlikuwa mdogo sana Gaza tulikuwa tunamwita Papa ni na kaka yangu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…