Mwanzo walikuwa wanasajili hivi:-
View attachment 61995
Mwenyekiti wa Simba akimsainisha Mbuyi Twite.
Hapa wamemaliza kazi,
Walipoona wenzao wanasajili hivi:-
View attachment 61997
Kisha wana:-
View attachment 61998
Ushahidi wa mchana kweupee,
Na wao sasa wameanza:-
View attachment 61999
Na kufikia mpaka huku:-
View attachment 62000
Naam hawa ndo Simba SC Mabingwa wa soka Tanzania ambao kwa kipindi cha hivi karibuni wamekuwa wakijaribu kuiga kila wanachofanya Kaka zao Dar Young Africans Mabingwa wa soka ukanda mzima wa Africa ya Mashariki na kati(Tanzania included)
Wameiga mengi sana,baadhi ni:-
Yanga ilipomchukua Kocha Kondic toka Serbia,Simba walimtafuta Milovan awamu ile ya kwanza.
Yanga ilipokwenda Uganda kumchukua Sam Timbe,Simba waka'do the same kwa kumchukua Mganda Moses Basena
Yanga ilivyomtimua Timbe na kurudiana na Papic(Mserbia),Simba na wenyewe wakamtimua Basena na kurudiana na Milovan(Mserbia).
Kuiga huku hakukuishia kwa makocha tu,kumekwenda hadi kwa Wachezaji Yanga walivyomsajili Davies Mwape(Mzambia) Simba wakatafuta Mzambia wao na kuangukia kwa Felix Sunzu, mwape ameachwa Yanga nafikiri kwenye dirisha dogo la usajili Simba wata'copy tena kwa Sunzu wao.
Ni jambo 1 tu ambalo Simba wamekuwa waki'struggle kuiga kwa miongo kadhaa sasa lkn wameshindwa nalo ni kutwaa Ubingwa wa Africa ya Mashariki katika ardhi za nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
All in all sifa pekee zimwendee Mpiganaji Abdalah Bin Kleb kwa kazi zake nzuri za kuwafunza Viongozi wa Simba namna ya kusajili kisomi,kwa mwamko huu wa kuiga yaliyo mema bila shaka msimu wa usajili wa mwakani Alhaj Rage atapunguza sana makosa yake ya kukosea wamiliki halali wa wachezaji wanaotaka kuwasajili baada ya kuchemka kwa Asamoah mwaka jana na Twite mwaka huu.
Nawasilisha!