Khamis Mgeja: Samwel Sitta lazima afukuzwe CCM

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,507
SIKU chache baada ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kutangaza timu inayoundwa na kundi lake kuwania urais 2015, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amesema chama hicho kinatakiwa kumchukulia hatua za kinidhamu kwa sababu anahatarisha uhai wa chama.

Alisema, kama chama kitamuacha aendelee kutoa kauli zinazohatarisha uhai wa chama, CCM itajiweka katika mazingira mabaya kisiasa pindi wapinzani watakapoanza kuchambua kauli hizo.

Kauli hiyo ya Mgeja, aliyoitoa jijini Dar es Salaam jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari, imekuja ikiwa ni siku chache tu tangu Sitta aitaje timu inayoundwa na kundi lake kuwania ukuu wa dola mwaka 2015.

Alisema wanaounda timu hiyo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, ambaye hata hivyo amekana kuwamo kwenye timu hiyo.

Jana akimzungumzia Sitta, Mwenyekiti huyo wa CCM, Mgeja alimshushia tuhuma nyingi akimwita mkorofi, mlalamishi na kwamba anaonekana wazi kukihujumu chama.

Mgeja pamoja na mambo mengine, alimshutumu Sitta kuwa alianzisha CCJ akiwa ndani ya CCM, kisha akataka kuhamia Chadema akiwa ndani ya CCM na yote hayo chama kiliyajua na kumwacha.

Alisema Sitta yeye ni waziri, lakini kuna wakati alikaririwa akisema kwamba, Serikali iwaombe radhi wananchi kwa sababu ya mgawo wa umeme, baadaye akasema maisha bora kwa kila Mtanzania hayawezekani na sasa amekaririwa hivi karibuni akisema Rais Kikwete alimhujumu kwenye uspika.

“Yaani anajiamini kiasi cha kuanza kumchokonoa hata Rais Kikwete, wakati akijua kwamba mambo anayoyafanya yanakwenda kinyume na mtazamo wa chama.

“Hivi huyu ni mtu gani asiyetosheka, kila wakati analalamika wakati yeye ni waziri na ana nafasi kubwa ya kupeleka malalamiko yake kwenye chama ili yakafanyiwe kazi.”

Alisema kama Sitta anaona yuko kwenye basi lenye abiria asioendana basi aondoke na kuhoji anafanya nini ndani ya CCM wakati anaonekana wazi kwamba haridhishwi na mwenendo wa chama na Serikali.

Mgeja pia alimtaka Sitta kwenda TAKUKURU kama anaona kuna rushwa ndani ya chama, au kama kuna wezi aende polisi na kama anaona kuna wahalifu, basi aende mahakamani.

“Lakini huyu mzee lazima chama kimchukulie hatua, huyu ni mzigo, kama hatadhibitiwa atakiharibu chama kwa sababu anaonekana ana ajenda ya siri,” alisema.

Mgeja aliitaka Kamati ya Maadili ya chama inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula, imjadili ili ijulikane ana ajenda gani.

Alisema kwa upande wake katika kikao cha NEC kijacho, atawasilisha hoja binafsi kutaka Sitta ajadiliwe.

“Yeye anajifanya ni msafi wakati mambo yake mengi tunayo, kwani hata alipopata uspika anaouota hadi sasa, alibebwa, tena kwa kampeni kali kweli kweli. Hivi, kwa nini asiwe kama mzee Msekwa (Pius Msekwa) ambaye baada ya kushindwa uspika alinyamaza kimya?” alifoka Mgeja.

Kwa mujibu wa Mgeja, kitendo kinachofanywa na Sitta ni cha hatari kwa uhai wa chama na kwamba kama isingekuwa huruma ya Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Rais Jakaya Kikwete, angeshafukuzwa uanachama wa CCM.

“Kuna wakati tulikaa tukataka kumnyang’anya kadi na aliokolewa na Mwenyekiti wetu, lakini pamoja na kusamehewa, bado hatulii, anaendeleza mambo yake ya ajabu ajabu,” alisema.

Akizungumzia kauli ya Sitta ya wiki hii aliyoitoa akiwataja Magufuli, Membe na Dk. Mwakyembe kwamba ni wasafi, alisema ni ya kibaguzi, kwa kuwa waliotajwa ni Wakristo, wala hakuna Muislamu hata mmoja.

“Aliowataja wote hao akiwa kanisani ni wakristo, wala hakuna Muislamu, wote hao ni wanaume na hakuna mwanamke, pia hao wote ni kutoka Tanzania Bara na inavyoonekana Unguja na Pemba hakuna watu safi.

“Sasa mtu kama anadiriki kusema uongo, tena madhabahuni, ana sifa gani ya kuwa kiongozi, yaani amefika mahali sasa anaanza ubaguzi wa Watanzania Bara na Visiwani, anaanza kubagua jinsia, huyu hafai na lazima achukuliwe hatua.

“Namtaka anyamaze, asiendelee na mambo yake kwa sababu kama ataendelea kupiga porojo, nitasema mengi zaidi yanayomhusu kwa sababu siyo msafi kama anavyotaka kuwadanganya Watanzania,” alisema.

Habari kwa hisani ya Mtanzania Jumapili.
 
Naishauri chadema....kitendo cha sitta kufanya anayoyafanya ni mbinu hatari kwa chadema. Sitta atafukuzwa ccm, atahamia chadema na huo ndio mwanzo wa kufa kwa chadema. Huu ni mpango ulioandaliwa makusudi,sio bahati mbaya...subiri na uone then CHADEMA jaribuni kumpokea Sitta na mwone atakavokuja kuwavuruga kipindi cha uchaguzi...DONT TRY IT...DONT TRY PLEASE! Hawa mashetani watawamaliza mkifanya hivo...
 
Watu kama Khamis Mgeja na Mh. Sitta niwa kuogopwa kama ukoma ndani na nje ya CCM. kama CCM kweli inataka kujipambanua kama hakina makundi na kama makundi yapo, lakini kinadhamira ya kuyafutilia mbali, basi hawa watu wanaolala huku wakiwaza uongozi wa juu kabisa wa nchi lazima wawapumzishe.

Huyu Mgeja ni wale wale. Anachokifanya hapa, ndiyo kile kile ambacho Mh. Sitta anakifanya. tofauti yake ni majukwaa wanayofanyia.

Kwanza uongozi wa CCM mkoa akiwa kama mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga umemshinda. Amesafiri all the way from Shinyanga kwenda kwenye majukwaa ya waandishi na wahariri wa habari Dar kumpiga vijembe Mh. Sitta. What a shame!.

CCM Shinyanga kwa sasa inachechemea kisiasa kwa sababu ina viongozi wa aina ya Mgeja, ambao ni wanafiki, wazandiki na hawajui kazi zao achilia mbali mipaka ya kazi zao.

Kwanza alibebwa na mwenyekiti wa CCM taifa hata kuupata tena uwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga. Is he paying FADHIRA?.

Watu wa aina ya mgeja ndiyo wapinzani wakubwa kwa CCM, na ndiyo hawa wanaoisukuma CCM polepole kutoka nje ya madaraka ya nchi kwa uroho na ubinafsi wao.

Kwa mstakabali wa CCM, kabla hawajaanza kufukuzana na vyama vya upinzani lazima kwanza wanunue ufagio wa nyumba na kufagia nyumba yao ili kuwafagia watu kama Mgeja otherwise, they have to get prepared for the inevitable to happen come 2014 & 2015.

Siyo ajabu watu wanawashangaa CCM kuwanyoshea vidole vyama vingine wakati wao nyumba yao haijasafishwa kiuongozi, kimaadili, kiheshima na pia kukosa ustahimilivu wa kisiasa.
 
huyu sita anazeeka vibaya kwa nini analia lia kila sku si ahamie chama sahihi au afufue CCJ Waliyoianzsha na kna nape wakaikmbia naskia alitoa adi furniture na ofsi jasri anayeogopa kivuli chake....ata uspka naskia walpmga msekwa zengwe aache wizi wa mchana Magufuli amemkana, mwandosya amemkana bado familia tu..kuna nn alichokuwa anakpata kwenye uspka mbona analalama sana huyu babuuuuuuu...mwizi mkubwa huyu
 
Haludzedzele; Wakiwa I.C.U wengine watajikuta CCJ na wengine CCM Origina Vs CCM Mpya.
 
Last edited by a moderator:
Haludzedzele; Wakiwa I.C.U wengine watajikuta CCJ na wengine CCM Original Vs CCM Mpya.Wote ni wanafiki watupu, huyo Mgeja anangoja nini kusema uchafu wa Sitta kama anaharibu chama?
 
Last edited by a moderator:
Wewe ngwamapala ni mtu wa sita ongea ualisia ccm shnyanga inatoka wap apa acha kutokwa mapofu sita anazeeka vbaya amna msafi wote wachafu mbona kna magufuli na mwandosya wamemruka huyu fsad sita.....akili ndogo haiwez kutawala akili kubwa
 
"Aliowataja wote hao akiwa kanisani ni wakristo, wala hakuna Muislamu, wote hao ni wanaume na hakuna mwanamke, pia hao wote ni kutoka Tanzania Bara na inavyoonekana Unguja na Pemba hakuna watu safi.

"Sasa mtu kama anadiriki kusema uongo, tena madhabahuni, ana sifa gani ya kuwa kiongozi, yaani amefika mahali sasa anaanza ubaguzi wa Watanzania Bara na Visiwani, anaanza kubagua jinsia, huyu hafai na lazima achukuliwe hatua.



Duuu, tumefika huko/ kweli sisiem ni janga la kitaifa, sikuhivi kila unapotaka kutoa sifa za watu kumbu ni lazima u-balance between dini, gender ubara na u-visiwani? sikujua hilo hakika.
 
Mbona mwenyekiti karuhusu makundi sasa ya nini kumwandama Sitta...
 
tusubiri tuone namna CCM italikataa jembe lake yenyewe
 
Naona ni mbinu chafu hizo za magamba na makundi ya kuhujumiana si.Sita wala Mgeja wanapaswa kuogopwa kama ukoma. Iweje mgeja amuongelee mwanachama mwenzake wakati yeye si msemaji wa chama ni mwenyekiti tena wa Mkoa fulani. Ilitakia tusikie kauri kutoka kwa mtu maalumu anayekisemea chama ambaye ni katibu wa habari na uenezi
 
Wewe ngwamapala ni mtu wa sita ongea ualisia ccm shnyanga inatoka wap apa acha kutokwa mapofu sita anazeeka vbaya amna msafi wote wachafu mbona kna magufuli na mwandosya wamemruka huyu fsad sita.....akili ndogo haiwez kutawala akili kubwa
Comment yako inaonyesha ni mmoja wa wale wale nimejaribu kuwaongelea kwenye bandiko langu la kwanza.

Jaribu kufuatilia comment zangu kujua ukweli kabla ya kuanza kupitisha kalamu kwenye jambo ambalo linahitaji kwanza utafiti.

CCM Shinyanga kwa kiasi kikubwa imebakiza majengo peke yake na siyo ajabu hata viti na mafaili kwa sasa yamejaa mavumbi kwa sababu hakuna anayefanya kazi kama inavyotakiwa zaidi ya kupiga majungu na uzandiki.

Mwenyekiti wa CCM mkoa amesafiri kwenda Dar kuongea na wanahabari badala ya kwenda kwenye vijijini kupata mawazo na maoni ya wanavijiji ili afahamu kwa nini waliamua kukinyima kura chama chake na kuwapa vyama vya upinzani.

He's well organised kwa kupiga majungu na uzandiki lakini pia his well disorganised katika utendaji wa kazi inayomfanya apate preveleges zote zitokanazo na kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
 
Chadema sasa hivi tuna funzo na bench mark hatupaswi kuwa jalala la kila takataka unless hizo takataka tuzifanyie recycling maana Shibuda na kina Shitambala watoshe kuwa vielelezo
 
Huyu Mgeja si ndo kibaraka wa wa Rostam na Lowasa? Na kama sikosei hii si mara ya kwanza kumshambulia Sitta. Nadhani naye anasumbuliwa na njaa tu
 
...
"Aliowataja wote hao akiwa kanisani ni wakristo, wala hakuna Muislamu, wote hao ni wanaume na hakuna mwanamke, pia hao wote ni kutoka Tanzania Bara na inavyoonekana Unguja na Pemba hakuna watu safi....
Kwa maoni ya Sitta, hao ni wasafi waliopo CCM, na sio waliopo Tanzania. Kwa maana nyingine ukiwataka watanzania wengine wasafi ambao pia ni wa dini nyingine, jinsia nyingine na kutoka upande mwingine wa Muungano inabidi uwatafute nje ya CCM
 
Hamis Mgeja yupo kundi gani linalotaka Urais 2015?. Upo kwa Membe, Migiro, Lowasa au upo kwa Steven Wasira?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…