Ahsante mwalimu wangu. Nimeshiba.Katika tamaduni za mazungumzo na maandishi, kinachotajwa mwanzo kwenye orodha ndicho kinachochukuliwa kuwa na uzito. Unaweza kukuta hicho kuwa ndio kimebeba dhima nzima ya mazungumzo au maandishi, hususan unapokiwekea na maneno ya kukuimarisha nguvu kama "Kwanza", "Awali ya yote,"
Mimi hakuna sehemu hata moja niliyosema sina tatizo
Katika jamii inayofuata utawala wa sheria kama yetu ya Tanzania, sheria za nchi ndio mwanzo wa kila kitu. Kwa hiyo uwepo wa katiba katika nchi yetu, tayari kunaipa umuhimu hoja ya uvunjaji wa sheria ukilinganisha na hoja ya "hajui kuoga" au "ananuka mkojo"
Gaijin,uko sawa kwa mtazamo na uelewa wako.Napenda nikuambie kuwa sio kila ambacho mtu anakizungumza na kuwa kweli sio lazima awe amefanya.
Pili,inasikitisha namna ulivyo na mawazo hasi kutokana na sababu nilizotaja hapo juu,badili namna ya kufikiri utaona ujumbe mzuri ulio nyuma ya thread yangu
pia pole kwa kuziumiza hisia zako inawezekana nimekukumbusha mambo ambayo uliyafanya huko nyuma na sasa unayajutia na unachagua kuwa na hasipa ili kukabiliana na majuto hayo!Pole kama nitakuwa sahihi na nitakua nimekutonesha,njia nzuri ni kusahau yaliyopita na kuanza maisha mapya!
Gaijin,uko sawa kwa mtazamo na uelewa wako.Napenda nikuambie kuwa sio kila ambacho mtu anakizungumza na kuwa kweli sio lazima awe amefanya.Pili,inasikitisha namna ulivyo na mawazo hasi kutokana na sababu nilizotaja hapo juu,badili namna ya kufikiri utaona ujumbe mzuri ulio nyuma ya thread yangu,pia pole kwa kuziumiza hisia zako inawezekana nimekukumbusha mambo ambayo uliyafanya huko nyuma na sasa unayajutia na unachagua kuwa na hasipa ili kukabiliana na majuto hayo!Pole kama nitakuwa sahihi na nitakua nimekutonesha,njia nzuri ni kusahau yaliyopita na kuanza maisha mapya!
Ndugu,
Nadhani wewe ndio wa kujiangalia vizuri. Thread umeiandika kwa haraka mno na nitakwambia kwa nini. Wewe umetoka ulikotoka(sijui nyumbani kwako au hotelini) na kuamua kufanya mazoezi. Ghafla unaona mtu mzima ''anamtoa''(sijui anamtoa kwenye nini geti au kopo) binti mdogo kama ''anamsindikiza'' kurudi ''kwao''. Haraka ukajenga imani kuwa atakuwa amelala nae. Hili ni kosa kubwa la kuhukumu unless unataarifa zaidi ambazo hujaziweka kwenye thread yako. Vipi kama hao ni mtu na mzazi au ndugu yake? Kwani kusindikiza mtu mpaka kuwe na uhusiano wa kimapenzi?
Madhara ya thread yako ni kuwa wachangiaji wenye haraka za kujibu tayari wanamshambulia huyo ''binti'' na hata wazazi wake pasi na lazima. Hebu jaribu kuiweka vizuri thread yako.
COMARADERIE,nilisema "inaonekana anakasindikiza kwao"
Kazi ya uzazi ni ngumu sana jamani.... As parents we try our best hoping kua wanetu wanakua katika maadili bora (atleast most of us do) BUT kitu kimoja I know from experience..... Wazazi ni watu wa mwisho kujua tabia mbovu za mtoto wao.... Kama mzazi mtoto akiingia kulala ana umri wa miaka 13, hivi kweli unaweza ukawa na wazo atatoka usiku? sio rahisi.....
Gaijin,hebu niambie,kusema kunuka mkojo ni kudhalilisha?Kusema ni wachafu ni kudhalilisha?Kusema hawajui mapenzi ni kudhalilisha?
Ni lazima kuna kitu kwenye akili yako kinakusumbua kama uko serious
Mkuu niliwahi kuwa na dada yangu hotelini tunakula akaja jamaa yangu baada ya kunisalimia akamgeukia sista na kumwambia hali yako shemeji-nilitamani ardhi ipasuke niingie!!!
Mazingira yanatosha kumtia mtu hatiani!
Soma upya uelewe!