Kesi ya Kafulila kuendelea Tabora Nov 3, 2016

chuuma

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2015
Posts
363
Reaction score
557
Rufaa ya Kupinga hukumu ya kesi ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma kusini kati ya David Kafulila(NCCR) dhidi ya Hasna Mwilima( CCM) iliyotolewa na Jaji F.Wambali ilitenguliwa Oktoba12 baada ya mapingamizi yaliyowekwa na upande wa pili wa mawakili wa serikali kwamba hati ya mashtaka ya Mhe Kafulila ilikua na kasoro za kiufundi.

Kutokana na kasoro hiyo,Mawakili wa Serikali waliomba Mahakama ifute moja kwa moja rufaa hiyo(dismiss)
lakini Majaji wa mahakama ya rufaa(Jaji Luanda, Jaji ?Mbarouk na Jaji Mziray)waliamua kutengua hati hiyo (struck out) kwa namna ambayo Kafulila anaweza kuamua kurejesha rufaa hiyo baada ya kurekebisha kasoro tajwa kwa hoja kwamba Mahakama haiwezi kuifuta moja kwa moja (dismiss)wakati haijafikia kusikiliza hoja za msingi wa rufaa yenyewe.

Kufuatia uamuzi huo, David Kafulila aliomba Mahakama kurekebisha kasoro hizo ili kesi ya msingi isikilizwe kuamua nani aliyeshinda uchaguzi wa jimbo hilo 2015 kwa mujibu wa fomu za matokeo 21B ambazo ingawa ziliwasilishwa na tume mahakamani huku kila upande ukidai umeshinda lakini Jaji aliyesikiliza shauri hilo ngazi ya Mahakama Kuu Jaji F.Wambali ambae siku chache baada ya hukumu hiyo aliteuliwa kuwa Jaji Kiongozi, aikataa fomu hizo kuhesabiwa ili kuamua mvutano huo.

Fomu hizo 21B zilipatikana baada ya Kafulila kuzidai hadi ngazi ya Jaji Mkuu baada ya Jaji Kiongozi ambaye ndiye aliyehukumu kesi hiyo kutomsaidia kuzipata kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Nikutokana na hatua hiyo ya Kafulila kufikisha maombi ya kutaka kesi ngazi ya rufaa iendelee, Mahakama leo imeagiza pande husika na kesi kufika mbele ya Jaji Mrangu Novemba3, 2016 Tabora kwajili ya ombi hilo lilowasilishwa na Kafulila ili rufaa iweze kuendelea.
 
Sio majaji wote wanatumika kupora haki naamini safari hii kafulila atatendewa haki
 
haki itapatikana tu...
ni dhahiri kuwa vipande vya noti vinatumika kama gundi kuzibia midomo waliopewa dhamana kutoa haki,..
 
Hakika hawa maccm watashindwa tu
 

Chuuma tuwekee kesi hiyo hapa tuone sheria ilivyodadavuliwa
 
hii kesi kafulila haweeezi na hatoweza kushinda...
 
hii kesi kafulila haweeezi na hatoweza kushinda...

Nakuhakikishia Kafulila atashinda rufaa yake easy!
Mahakama iliyo sikiliza kesi chini ya Jaji Wambali ilikataa kupokea forms kutoka vituo vyote vya uchaguzi ili kuziangalia upya!Kukataa zile hati ilikuwa ndiyo mwisho wa kesi ile
Lkn Mahakama ya rufaa imekubali kuzipitia zile form ambazo ndiyo msingi wa kesi ya Kafulila
Hata CCM Kigoma sasa wanajua kuwa ngoma
Inogile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…