Wanajukwaa,
Nilikuwa mwanaccm miaka ya nyuma 1990_2000, nilikuja kukisusa chama hicho kuanzia mwaka 2007 kwa kuona hakikidhi yale ninayoyahitaji, tangu hapo nikaanza kutafuta upande ambao upo salama kidogo ili nishirikiane nao katika kuijenga Tanzania bora,
Mnamo mwaka 2010, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kilionesha ukomavu wake na ndipo nilipoanza kukiunga mkono ila sikuwa mwanachama, kwa mwaka huu nimeshirikiana nao kampeni kikamilifu na wamenifurahisha kwa kampeni safi walizofanya hasa mgombea wao wa Uraisi
Mh Edward Ngoyai Lowassa,
Kwa akili zangu timamu, nikitambua umuhimu wa kuwa mwanachama kwenye chama bora, bila kulazimishwa na mtu yeyote, kesho nitaachana rasmi na Ccm na kuwa mwanachama
halali wa Chadema, chini ya mwamvuli wa UKAWA.
Sitakushangaa sana wewe uliyebaki Ccm leo hii kwani kila mtu na mtazamo wake ila ninachokiamini, miaka mitano ijayo utakuwa umerudi kwenye mstari kama mimi.
Tukutane kesho jangwani.
Mungu Ibariki Tanzania.
youngsharo