Kero ya Foleni Dar

PeaceLover

Member
Joined
Oct 21, 2012
Posts
7
Reaction score
1
Inawezekana kabisa foleni tunayokutana nayo hapa mjini si kwa sababu eti barabara ni nyembamba tu hapana!
Kuna mambo kama vile wasimamia sheria za barabarani (Traffic police) kutojipanga vema kuweka utulivu kwenye barabara zetu. Mfano ukiwa katikati ya mji utawakuta traffic wamekaa kona hata wa4 au zaidi wakati sehemu zingine za pembezoni kidogo ya mji kama vile mbagala, kimara, mbezi, tegeta nk. ambako ndiyo kwenye vurugu zaidi HAWAPO kabisa! Suala lingine ni ukosefu wa uvumilivu kwa madereva wasiokuwa na busara za kazi yao. Utakuta barabara ina lane 1 ya kwenda na 1 kurudi, sasa mkiwa kwenye foleni kuna wajanja (mi nawaita wajinga tu) wanachomoza na kupita kwenye lane inayopaswa kutumika kwa magari yanayotoka upande wa pili na kwenda kuchomeka mbele ya wenzao huku wakiwa wamefunga njia ya upande mwingine! Jamani huu ni UJINGA wa aina yake.

Rai yangu ni kwamba:
1. Jeshi la polisi lihakikishe linasambaza askari wa kutosha barabarani ili kukabiliana na madereva wajinga wanaofunga njia na kusabaisha msongamano usiokuwa wa lazima.
2. Madereva mzingatie taaluma zenu na kuwa na busara zaidi hasa ukifikiria watu wote wanaharaka ya kufika waendako.

Karibuni wadau kuchangia hoja.
 
Sababu kubwa ya foleni Dar ni traffic police kuongoza magari kwenye taa na kushindwa kuwadhibiti wanaondesha kwenye mabega (watanuaji). Hivi hatuna vyuo hapa chini wakafanya utafiti kuthibitisha kuwa kwa hali tuliyo nayo sasa taa ni bora zaidi kuliko askari maana kuna even distibution ya magari kwenye barabara zote kuu, tofauti na zamani ambao magari yalikuwa mengi baadhi ya barabara hivyo traffic police walikuwa wanasaidia kubalance hilo. Taa ni bora zaidi inakufanya usichoke- psychology of queuing inaonyesha ukiwa unasogea kidogo kidogo kwa dk 30 ni bora zaidi kuliko kusubiri dk 30 ndio uvuke kwa mara moja
 

Mkuu nakubaliana na wewe 100% foleni yetu inasababishwa na traffic polisi na ujinga wetu madereva. Kwenye makutano ambako hakuna mataa tunashindwa kufuata sheria za barabarani. Tatizo kubwa Tanzania waendesha magari wengi si madereva. Mara ngapi unaona watu wanapita kulia mwa round about eti wanawahi. Kwenye round about watu hawajuhi nani ana righ of path.
 
Aisi. hapa ngoja nipite tu.. kwa hiyo madereva Na traffic police ndio wanasababisha foleni!
 
Suluhu ni kujenga flyover walau nne tu kwa kuanzia ubungo magomeni tazara veta-changombe na

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwa kuanzia nadhani tuanze na kukomesha tabia za madereva wakorofi kwanza, badala ya kuwaachia au kuwalipisha fine ni bora dereva akikamatwa na makosa ya kijinga kama kutanua au daladala kupakia katika foleni anaenda jela wiki 2 bila kujali ni nani wala nani
 

Mbona zamani hapakuwa na kero ya foleni? Au madereva hawakuwepo? Au trafic hawakuwepo? Insu niserekali na miundombinu yake hawana mipango endelevu, wanangojea tatizo liwe kubwa ndo waanze kuhangaika, population iliopo dar haijatokea ghafla, kila mwaka watu wanaongezeka! Na miundombinu nayo inatakiwa irekebishwe ili iendane na ongezeko la watu, angalia daraja la kigamboni limeongelewa miaka mingi mpaka leo! Walisema watajenga barabara ya kupita juu na chini pale tazara badala ya mataa, mpaka leo ni stori tu itapita hata miaka 10! Wameanzisha usafiri wa treni badala ya nauli kuwa chini kuliko ya bus imekuwa juu! We umeona wapi duniani nauli ya treni ikawa juu zaidi ya bus? Hao matrafic wenyewe wanachoangalia ni nani kakosea wapate kula, hayaaa'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…