Ninampango wa kuhama hili jukwaa la Kenya siku za karibu, sitoendelea kuchangia kwasababu ya kiwango kidogo cha uwelewa wa mambo mnachokionyesha ninyi wakenya, haina maana kama mtu anatoa comment bila kuifanyia utafiti wa kina, Miradi yote mnayoipoteza sababu kubwa sio Tanzania.
Rwanda ilikua tayari kuunganisha na Kenya, lakini Uganda ilisema haitokuwa na uwezo wa kujenga vipande vitatu kwa wakati mmoja, hivyo walichagua kuchagua Kampala kwenda Juba badala ya Kigali kutokana na ukubwa wa biashara kuwa mkubwa kuliko ule wa Rwanda na Uganda, Rwanda haikua na choice nyingine zaidi ya kuigeukia Tanzania, je Tanzania inahusikaje katika hilo?