mchambawima1
JF-Expert Member
- Oct 16, 2014
- 2,487
- 738
Hongera polisi wa Rwanda, naskia huwa hawahongwi. Polisi wetu wa Kenya wajifunze jambo kutoka kwa hawa Wanyarwanda. Polisi wa Kenya na Tanzania ndio huwa kama waliumbiwa jehanamu. Hebu siku moja endesha gari lenye nambari za usajiri wa Kenya kuanzia Namanga hadi Dar es Salaam, ndio utakoma, yaani utaomba heli uliache Dar lifie huko na urudi kwa bus.
Ninge shangaa umalize post bila neno Tanzania!! ila leo kauzalendo umekaweka pembeni kidogo japo umesahau kuelezea na wa tanzania akija na gali huko atatamani aliache gari Nairobi na kupanda NDEGE
Mambo ya uzalendo ni yenu na ujamaa, kama kitu kibovu ni kibovu na siwezi tetea ujinga, kuna tofauti kubwa sana kati ya Mkenya na Mtanzania, nyie mpo vipofu kwa uzalendo hata wakati mnatafunwa hadi mifupa. Siwezi bisha ukisema polisi wetu walikuzingua maana nawaelewa ni washenzi na wapumbavu sana. Wana tuhuma za kuhongwa na kuwaacha Alshabaab waingie mipakani.
Ninachofahamu ni kwamba, unapoendesha gari lenye nambari ya Kikenya ukiwa Tanzania, bora uhakikishe muda wote upo nyuma ya gari la Kitanzania maana jamaa wakiona tu nambari za kigeni, basi mara moja wanajua hela ndio hizo, hata gari liwe sawa vipi na stakabadhi zote. Unaskia eti hela za maji.
Tatizo lako wewe #Lawmaina78 wazamani wewe unakachuki kiasi na watanzania, hata tungekuwa vipi huwezi kutusema vizuri kamwe, ila nakueleza wacha kutuita vipofu kama tulikua vipofu nizamani na sileo, hebu rudia kutembelea Tanzania yaleo lazima utagundua si vipofu tena ndegu.