Mwl Kichuguu, Nyani(sio nyani ngabu) haoni makalio yake...Najua wakenya watajaribu kurefute hiyo report.
Babuu eeh,
hakuna mkenya in his/her right mind atakayebisha na hii kitu otherwise
itakua denial.Asilimia kubwa ya wakenya ni masikini na wanasota kinoma.
Kutajirika kwa wachache haimanishi eti nchi imeendelea...ila wezi wamezidi.
Zile kura za mwaka jana brought to light the fragility of the Kenyan fabric
na nyote mlishuhudia.Kibaki amjilazimishia madaraka na amewanufaisha
wapambe wake huku raia wanalia njaa maana bei za bidhaa zimeruka
kishenzi na hazish'kiki.Hebu fikiria kama wiki mbili tatu ziilzopita unga wa
ugali ulikua unauza anywhere between 80 to 120 Ksh.Ni wazi kua bei
halali ni 45 Ksh.Mabepari wanawaibia walalahoi na serikali imeichuna tu
kana kwamba hamna chochote kinachoendelea.
Kisha kuna posti moja nilitundika humu kuhusu vile askari jela wanavyoishi
na how that translates into the care the give to the inmates.Yaani ni unyama
juu ya unyama mpaka unashangaa hawa watu vipi jamani.The social fabric
ambayo kwamba Kenya ilikua inajivunia, imefanywa mararu na issue za
kijamii kama hizi.Kulikua na kipindi wanafunzi wa shule za sekondari walifanya
migomo na kuanza kuchoma mabweni and any other school property just
to vent their frustration at mock exams.
Mwalimu mmoja wa saikolojia akasema kua the students were reflecting
what Kenya had become after the elections of 2007...or maybe that was
just what they were na watu walikua hawajui ukweli wa hali halisi.