Priorities za waafrika zinachekesha sana, nchi ambayo wananchi wake wanakufa kila siku kutokana na uhaba wa chakula wanatumia mabilioni kwa ajili ya mtandao. Na kuna watu hapa wanashangilia hapa wanayaona hayo ni maendeleo...
Mkuu, bila shaka wataikumbuka Tanzania wakati walipo pata baa la njaa nchini mwao mahindi yetu yaliwasaidia sana, hii ndio maana alisi ya kuwa na jirana mwema. Kuna Wakenya wengine wanajua sana kujieleza vizuri na kuleta vitu vyenye substance - chukulia mtu kama
Livefire, Smatta, Moto na Mzallendo ingawa wakati mwingine wanatumia lugha kali lakini unajuwa wakati mwingine wako
sincere. Inapokuja kwa wale waliobaki unashindwa kabisa kuwaelewa, leo watasema ni Wakenya kesho ni Watanzania kuna thread fulani niliwahi kuisoma humu ni mtu racist vibaya sana yaani niki-reproduce humu Wakenya na Blacks wote duniani watashtuka sana, msimuone hapo huyu jamaa anatumia lugha za ki-neo NAZI ana mawazo ya
kishetani kuliko Hitler, kila mtu mweuzi yeye anamuona ni takataka tu; we sema tu is a
master of disguise kwenye forum hii anajifanya kuwa binadamu lakini deep down ni mtu
racist wa kutupwa! Angekuwa Tanzania mimi nige-press charges dhidi yake I mean IT, kuna wakati fulani Mkenya mwenzake alimuonya lakini kwa bahati mbaya naona watu hawakumuelewa, nikitoa mambo anayo andika ndiyo mtamuelewa.
Mara zote huwa anahanzisha thread alafu baadae anatumia thread hiyo hiyo kuisema vibaya TANZANIA mtu unashindwa kumuelewa anachotaka ku-put across ni nini hasa au kina manufaa gani katika nchi zetu za Africa Mashariki, badala ya kuleta mambo mazuri ya kushauriana na kuelimishana kama majirani, wanapoteza muda kuleta mambo ya kitoto tu eti sijuhi Kenya imefanya nini! itawachukua Watanzania light years kupata mafanikio kama hayo, akili zake ziko katika mambo ya ushindani usio na mantiki yoyote! Niliwahi kuwambia kwamba hata America illikuwa na jeuri na majigambo kama haya lakini sasa hivi hiko wapi - wanakwenda kuwaomba msaada wa kipesa Wachina si hilo tu juzi juzi Wamerikani wakawapeleka Wakuu wa majeshi wa China kwenye kituo chao cha Navy (
sina uhakika ni kituo gani) Wamerika wakawa transparent na kuwaonyesha Wachina silaha zao, si hilo tu wakawaomba Wachina wasiwe wanaigilia mifumo ya kompyuta zao kupitia kwenye internet, hii nafikili ingekuwa SOMO tosha kwa majirani zetu kwamba mnaweza kufikili wenzenu wamelala usingizi, kweli kuna vitu tulikuwa tuna-lag behind not anymore tunajipanga vizuri tu na serikali yetu hilo imekwisha ling'amua inalifanyia kazi, vile vile nataka kuwakumbusha kwamba Tanzania wapo wataalamu mahili sana wa kuheshimika. Kuna Mkenya mmoja alifikili Tanzania hakuna wataalamu wa kujenga barabara, mambo ya ajabu SANA!
Back to the point, nataka kuwafahamisha kwa kifupi wenzangu kwamba mwaka jana kampuni ya WaTanzania wafanya biashara alihanza kufunga vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya mawasiliano wakitumia (WiMax na LTE) kampuni inajulikana kama
4G mobile TZ, ni kampuni ambayo inamilikiwa na wazawa 100% na ndiyo itakuwa ya kwanza kutumia broadband kwa ajili ya DATA na VOICE nchini Tanzania. Kampuni hii inategemea kupunguza gharama za mawasiliano, kutoa kasi nzuri ya throughput yenye kiwango cha kuanzia 70 Mbps on down link and 30 Mbps on up link, tekinolojia itakayo tumika ni Wimax na LTE. Ninacho taka kusema hapa ni kwamba siyo kwamba Tanzania haijuhi kwenda na wakati tunafanya vitu kimya kimya bila ya makuu, hii ina maana Kenya itakuwa nchi ya pili katika East Africa kuafata mkondo huu - siyo kwamba ndio mlio anzisha.
Hizi tabia za ku-dramatise mambo as if 4G tekinolojia ya ajabu sana, kwa hiyo itakuwa confined tu kwa nchi zenye uwezo sijuhi nini ni kitu cha kushangaza sana, na kinakuwa kibaya zaidi mtoa habari anapokuwa mbumbumbu katika tekinolojia ya mawasiliano wanazungumza chochote kinacho wajia kichwani bila ya kufanya utafiti, kwani haya mambo ya 4G iwe LTE au Wimax mbona ni mambo ya kawaida sana Taifa lolote linaweza ku-roll out teknolojia hii muda wowote wakitaka. Labda nimkumbushe kwamba si Tanzania, Kenya au Uganda wenye uwezo wa kuhunda vifaa hivi vya mawasiliano wote tunanunua kutoka aidha Uchina kwenye makampuni ya Hauwei au ZTE na huko Ulaya vinapatikana kutoka Ericsson ya Sweden hela yako tu. Muache tabia ya kuwa mna-blow vitu out of proportion.