Mkuu, Kuna huu ushoroba wa kati unaufuatilia vizuri?. SGR itaongeza ufanisi wa bandari ya Dar na Tanga by 100%.
Mkuu, hivi huoni jinsi Burundi, DRC na Uganda wanavyohangaika kuhusu hii reli?. Tukiachilia mbali mizigo mengine ya ndani, bandari ya Dar pekee ikitumiwa na hizi nchi tatu by 80% na Uganda na South Sudan by 50% ya mizigo yao ya hivi Sasa tu, tunauwezo wa kupata mapato ya nchi nzima by 50%.
Lengo la hizi nchi kukimbilia Sana hii SGR ni kutaka kuanza kichimba madini yao mazito ambayo kwa Sasa hawawezi kuyachimba kwasababu hawawezi kuyasafirisha nje ya nchi. Kwahiyo usiangalie miaka 5 ijayo, huu ni mradi utakaodumu miaka 100 ijayo. Huu mradi "stimulating effect on the economy" ni mkubwa Sana mkuu, hasa kwa DRC, Burundi na Uganda.