Ajibu alicheza Simba ya mfumo tofauti kiuongozi na kimchezo.
Kwa Simba ya sasa ni vizuri ijiridhishe kuwa wachezaji waliopo wameanza kutambua maana ya kuwa quasi-professional. Principally, Ajibu alionekana kama amebadilika sana alipoenda Yanga hasa kinidhamu, kama alivo maintain performance kwa muda mpaka hapa karibuni. Inashangaza amekorofishana nini na Yanga zinaanza tena stori za kwenda Simba.
Simba ya sasa inaanza kuwa na culture ya kimataifa. Kama anarudi Simba, wana intelijensia wahakikishe yeye na mswahiba wake waliobaki Simba, hawawezi kuanzisha vimambo mambo vya kuturudisha nyuma.
My suspicion is that, Yanga wamekata tamaa naye kwa kuwa walitegemea angeifunga Simba ili iwe scandal kubwa. Kwa kuwa imeshindikana, hawaoni umuhimu wake sana.
Simba inaweza kumpokea kama watajiridhisha kuwa ana moyo wa dhati kuchezea Simba. Umri unaruhusu kuipa mafanikio. Aliwahi kuondoka Mambosasa, kabla ya ligi ya klabu bingwa tukacheza mpaka raundi ya tatu ndiyo akarudi, tunacheza na mabingwa watetezi: Accra Hearts of Oak, akafanya maajabu tukaenda mpaka semi-final.
Aliendelea kuisumbua Simba, On and Off, lakini enzi hizo walikuwepo watemi kwenye timu kina Jumanne Masumenti (De Nascimento), ndiyo walikuwa wanammudu.
Alidumu Simba, na Nigeria Afcon alikuwepo na aliendelea kuwa karibu na Simba maisha yake yote. Naamini hiyo inaweza kuchukuliwa kama vitu vya kupita tu, apokelewe tena, kama kweli Ajibu ni mpezi hasa wa Simba.