Ilikuwa baraka kubwa sana kwa nchi ya Kenya kumpata rais kama Emillio Mwai Kibaki, baada ya utawala wa kiimla wa dikteta Arap Moi kwa miaka 24. Bure tungekuwa bado tumepotea njia hadi muda huu. Kama kijiti kingepokezwa kwa kiongozi asiyejielewa au yule ambaye angeamua kufata nyayo za 'Nyayo'. Aliilekeza Kenya mpya kwenye mkondo ambao umetufaidi sana.
Akahakikisha kwamba amefanikisha shughuli yote ya kupata katiba mpya, mihimili nayo akaiimarisha. Taasisi mpya na huru za kiserikali nazo akazibuni, kisheria, chini ya muongozo wa katiba hiyo mpya. Zaidi ya yote, kwa ushirikiano na viongozi kama RAO na wengine, ambao hata hawakuwa wanaelewana kisiasa, akatuacha na ruwaza hii ya Kenya Vision 2030.
Leo hii wote wanaogombea kiti cha urais na nafasi zingine. Hata wale ambao wanaonekana kwamba hawana hope kabisa ya kutimiza ndoto zao, wanazungumzia sera ambazo zipo 'based' kwenye ruwaza hiyo. Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, licha ya mapungufu yake kadhaa, amefanikisha kutimiza mengi yaliyotajwa kwenye Vision 2030. Tena kabla ya muda na deadline zilizonuiwa kwenye ruwaza hiyo.
Kenya vision 2030 imetupaisha hadi kimataifa pia. Baada ya kutimiza malengo mengi, ambayo yaliafikiwa kwenye mikataba na makubaliano ya kimataifa. Tulipoingia kwenye milenia mpya mwaka wa 2000. Malengo ya kimaendeleo ambayo yalijumuishwa moja kwa moja kwenye ruwaza hiyo. Almaarufu kama MDGs(Millenium Development Goals).
Leo hii Kenya ina sifa kimataifa, kama nchi ambayo inatekeleza ahadi zake na imezipiku hadi nchi ambazo huwa zinajiita '1st world'. Kwa mfano ikifika kwenye masuala ya mazingira na nishati mbadala. Kenya ni kati ya nchi zinazo ongoza barani Afrika na inatajwa kwenye orodha ya nchi 'top ten' duniani.
The country was praised for its extensive renewable energy value chain.